27 Juni 2026 - 16:40

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, kufuatia kuuawa shahidi kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Sayyid Ali Khamenei, na kutokana na maombi ya mara kwa mara ya wanazuoni, viongozi wa makabila na wasomi wa Iraq, miji mitakatifu ya Najaf na Karbala inajiandaa kupokea mamilioni ya waombolezaji katika mazishi ya kihistoria yatakayofanyika tarehe 8 Julai.

Shirika la Habari la la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Iraq imeanza maandalizi makubwa kwa ajili ya mazishi ya kihistoria na ya mamilioni ya waombolezaji kufuatia kuuawa shahidi kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Sayyid Ali Khamenei.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, baada ya maombi ya mara kwa mara kutoka kwa wanazuoni wa Kiislamu, viongozi wa makabila na wasomi wa Iraq, imeamuliwa kuwa mazishi ya mwili mtukufu wa kiongozi huyo yatafanyika siku ya Jumatano, tarehe 17 Tir 1405 kwa kalenda ya Iran, inayosadifu tarehe 8 Julai 2026, katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kidini nchini Iraq wameeleza kuwa tukio hilo linatarajiwa kuwa miongoni mwa mikusanyiko mikubwa zaidi katika historia ya kisasa ya eneo hilo kutokana na nafasi ya Imam Khamenei katika ulimwengu wa Kiislamu na mhimili wa mapambano dhidi ya ubeberu na Uzayuni.

Katika maoni yake, mwandishi maarufu wa Iraq, Muhammad Sadiq Al-Hashimi, alisema kuwa mwaka huu Waumini wa Kishia nchini Iraq wameunganisha kwa hiari yao maombolezo ya Ashura ya Imam Hussein (as) na msiba wa kuuawa shahidi kwa Imam Khamenei.

Aliongeza kuwa mshikamano huo ni ujumbe wa wazi kwa Marekani na Israel kwamba ndoto ya kuvunja uhusiano wa kindugu na wa kimkakati kati ya Iran na Iraq haitatimia kamwe.

Maandalizi katika miji ya Najaf na Karbala yanaendelea huku mamilioni ya waombolezaji kutoka Iraq na mataifa mbalimbali yakitarajiwa kushiriki katika mazishi hayo ya kihistoria.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha