3 Julai 2026 - 12:55
Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Iran: Nchi za Kiislamu Lazima Zizuie Israel Kuchochea Mvutano Mashariki ya Kati

Waziri wa Ulinzi wa Iran (akikaimu), Brigedia Jenerali Majid Ibn al-Ridha, amesisitiza umuhimu wa kuanzishwa kwa mfumo wa pamoja wa kiusalama kati ya nchi za Kiislamu ili kuzuia utawala wa Israel kuchochea mivutano katika eneo la Mashariki ya Kati.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, akikaimu, Brigedia Jenerali Majid Ibn al-Reza, ametoa wito kwa nchi za Kiislamu kuunganisha nguvu na kuanzisha mfumo wa pamoja wa kiusalama utakaoweza kuzuia utawala wa Kizayuni kuchochea mivutano katika eneo la Mashariki ya Kati.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa mazungumzo ya simu kati yake na Waziri wa Ulinzi wa Turkey, Yaşar Güler, ambapo viongozi hao walijadili hali ya sasa ya kikanda, utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano, pamoja na njia za kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na kiusalama kati ya nchi hizo mbili.

Aidha, Brig. Gen. Ibn al-Ridha amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekubali makubaliano ya kusitisha mapigano kwa lengo la kusaidia kurejesha utulivu wa kikanda, kufuatia ombi la nchi rafiki na jirani. Hata hivyo, ameonya kuwa Tehran haina imani kamili na upande wa pili kutokana na historia ya kutotekelezwa kwa makubaliano na Marekani.

Ameongeza kuwa vikosi vya jeshi la Iran viko katika hali ya utayari kamili na vitajibu kwa uwiano wowote wa uvunjaji wa makubaliano, huku akisisitiza umuhimu wa tahadhari na mshikamano wa nchi za Kiislamu katika kulinda usalama wa kikanda.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha