Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Uongozi wa Ataba Tukufu ya Imam Hussein (a.s.) umetangaza kuwa umekamilisha maandalizi yote ya kiutawala, kiusalama na kihuduma kwa ajili ya kupokea msafara wa mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Hussein Khamenei (Quddisa Sirruh).

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Sekretarieti Kuu ya Ataba hiyo, mazingira ndani ya Haram Tukufu ya Imam Hussein (a.s.) yameandaliwa kwa ajili ya kufanyika kwa swala ya janaza, ambayo itaongozwa na mwakilishi wa Marjaa Mkuu wa Kidini, Ayatullah Sayyid Ali al-Sistani, ambaye ni Sheikh Abdul Mahdi al-Karbala'i.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa njia za kupita msafara wa mazishi na washiriki zimeandaliwa kikamilifu, huku timu za huduma na matibabu zikiwa zimewekwa tayari. Aidha, mipango maalumu imefanywa kuratibu uingiaji na utokaji wa waombolezaji ili kuhakikisha shughuli hiyo inafanyika kwa utulivu na mpangilio mzuri ndani ya Haram Tukufu ya Imam Hussein (a.s.).

Your Comment