Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Naibu Kiongozi wa Jamaat-e-Islami Pakistan, Liaqat Baloch, amesema Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei (r.a.) aliiongoza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa miongo kadhaa akiwa mwaminifu kwa misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu, na kufanikiwa kuifanya Iran kuwa taifa lenye mshikamano na mapambano dhidi ya Uzayuni na ukoloni.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Shirika la Habari la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRNA) kandokando ya shughuli za mazishi ya Kiongozi Shahidi mjini Tehran, Baloch alisema Imam Khamenei alidumisha msimamo wake bila kuyumba mbele ya shinikizo la Uzayuni na ubepari wa kimataifa.
Aliongeza kuwa Kiongozi Shahidi alikuwa na ujumbe wa wazi wa kuhimiza umoja wa Umma wa Kiislamu na aliendelea kuiunga mkono kwa dhati harakati ya ukombozi wa Palestina, akieleza kuwa wananchi wa Iran watabaki kuwa chanzo cha hamasa kwa mataifa mengi duniani.
Baloch pia alisema kuwa licha ya Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya kutumia mabilioni ya dola katika juhudi za kuidhoofisha Iran, uongozi wa Imam Khamenei uliimarisha ustahimilivu wa wananchi wa Iran na kuujenga umoja wao katika kushikamana na misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu.

Wakati huo huo, shughuli za mazishi ya Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei zimeendelea katika miji mbalimbali mitakatifu, ambapo baada ya kufanyika kwa mazishi makubwa mjini Tehran yaliyohudhuriwa na mamilioni ya waombolezaji, msafara wa mazishi umeendelea katika miji ya Qum, Najaf, Karbala na Mashhad.
Your Comment