9 Julai 2026 - 21:10
Kamanda Abdollahi: Tutawalipiza Kisasi Waliomuua Kiongozi Shahidi Sayyid Ali Khamenei (ra)

Kamanda wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya (s), Luteni Jenerali Ali Abdollahi, amesema Iran itaendelea kufuatilia na kuwaadhibu waliomuua Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeuawa shahidi pamoja na mashahidi wengine.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Kamanda wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya (s), Luteni Jenerali Ali Abdollahi, amesema kuwa huzuni na hasira iliyopo miongoni mwa wananchi wa Iran kufuatia kuuawa kwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeuawa shahidi zitaendelea hadi pale waliotekeleza mauaji hayo watakapoadhibiwa.

Katika taarifa yake iliyotolewa Alhamisi, Abdollahi alisema kuwa azma ya kulipiza kisasi kwa wauaji wa kiongozi huyo, ambaye alimwelezea kuwa kiongozi wa Waislamu na watu huru duniani, pamoja na mashahidi wengine waliouawa katika vita vya hivi karibuni, itaendelea bila kuyumba.
Kamanda huyo alieleza kuwa dunia ilishuhudia katika siku zilizopita tukio la kihistoria na la kipekee kupitia mazishi na shughuli za kumuaga Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, akisema kuwa tukio hilo litaendelea kubaki katika kumbukumbu za historia.

Aidha, alisema kuwa mazishi hayo yalimdhihirisha kiongozi huyo kama alama ya busara, imani, jihadi na muqawama (mapambano ya upinzani), na kusisitiza kuwa fikra na njia yake vitaendelea kuishi katika nyoyo za wafuasi wake na katika historia ya ulimwengu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha