12 Julai 2026 - 01:03
Wizara ya Usalama ya Iran Yapongeza Mahudhurio Makubwa ya Umma wa Kiislamu Katika Mazishi ya Kiongozi Shahidi

Wizara ya Usalama ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa taarifa ya kupongeza ushiriki mkubwa wa wananchi, Marjaa wa dini, serikali na wajumbe kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu katika mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, ikieleza kuwa tukio hilo limeonyesha umoja, uaminifu na mshikamano wa Umma wa Kiislamu.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Wizara ya Usalama ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa taarifa rasmi ikieleza shukrani na pongezi kwa ushiriki mkubwa wa wananchi, Marjaa wa dini, serikali na ujumbe kutoka mataifa mbalimbali ya Kiislamu waliohudhuria mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei (Mwenyezi Mungu amrehemu).

Katika taarifa yake, Wizara hiyo ilinukuu Aya ya 23 ya Suratul Ahzab inayosema: "Miongoni mwa Waumini wapo watu waliotimiza ahadi waliyoahidiana na Mwenyezi Mungu. Wapo waliotimiza wajibu wao, na wapo wanaongoja, wala hawakubadili ahadi yao hata kidogo."

Taarifa hiyo ilieleza kuwa mazishi hayo makubwa na ya kihistoria ya mwanazuoni mpambanaji na kiongozi mwenye hekima wa Muqawama yalikuwa ishara ya kudumu ya uaminifu, utambuzi na mshikamano wa Umma wa Kiislamu, pamoja na kuthibitisha upya kujitolea kwa misingi ya Kiislamu na maadili ya Mapinduzi ya Kiislamu.

Aidha, Wizara ya Usalama ilisisitiza kuwa mahudhurio makubwa ya wananchi wa Iran na Iraq yalidhihirisha kwa mara nyingine kina cha udugu na uhusiano wa kidini na kijamii kati ya mataifa hayo mawili.

Vilevile, taarifa hiyo ilivisifu vikundi vya makabila, vijana wa Iraq na taasisi za kidini chini ya uongozi wa Marjaiyya kwa mapokezi yao, ukarimu na mchango wao mkubwa katika shughuli za mazishi, ikieleza kuwa matukio hayo yamekuwa urithi wa kudumu wa mshikamano na undugu wa Umma wa Kiislamu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha