Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Naibu Gavana wa Mkoa wa Fars anayeshughulikia masuala ya usalama na kijamii, Ahmad Ahmadizadeh, amesema kuwa ndege za kivita za Marekani zilifanya mashambulizi ya anga katika maeneo ya miji ya Kazerun na Farashband, kusini mwa Iran, alfajiri ya Alhamisi.
Ahmadizadeh amesema kuwa mashambulizi hayo, yaliyofanyika katika saa za mwanzo za alfajiri, hayakusababisha vifo wala hasara ya maisha ya binadamu, kwa mujibu wa taarifa ya mamlaka ya eneo hilo.
Amesema hali katika miji hiyo kwa sasa iko shwari na ya kawaida, licha ya mashambulizi hayo ya anga.
Maoni yako