Kikundi cha Magaidi wa Daesh wamesambaza video inayoonyesha kuchinjwa kwa raia wa Marekani,Peter Kassig alikuwa miongoni wa wasamaria waliokuwa wakitoa misaada ya kibinadamu kwa waathirika wa vita.
Video hiyo inamuonyesha mawanamume mmoja anayeonekana kuwa mwanachama wa Islamic State akiwa na kisu mkononi na maandishi yanayosema kuwa Peter Kassig ameuawa.
Kanda hiyo pia ina picha za watu kadha waliouawa ambao wanasemekana kuwa wanajeshi wa Syria waliokuwa wametekwa nyara.
Marekani imesema kuwa inafanya juhudi za kubaini chimbuko la kanda hiyo.
Bwana Kassig ambaye anajulikana kama Peter alitekwa nyara mwaka uliopita.
Mnamo mwezi Octoba kanda nyengine ya video ya kifo cha mfanyikazi mwengine wa misaada kutoka Uingereza Alan Henning iliisha huku Kassig akitishiwa.
Magaidi wa Daesh wamekuwa wakiua makundi ya watu kila kukicha, na kufanya jinai ambazo hazijawahi kuonekana katika mashariki yakati.
16 Novemba 2014 - 13:36
Msimbo wa Habari: 651731
Kikundi cha Magaidi wa Daesh wamesambaza video inayoonyesha kuchinjwa kwa raia wa Marekani