Jamhuri ya kiisalamu ya Iran imesema itapinga shinikizo lolote la mataifa ya magharibi litakalo lenga kuifanya ikubali masuala magumu na yasiyokubalika katika mazungumzo kuhusu mpango wake wa nyuklia.
Mazungumzo ya mwisho kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran yalianza jana mjini Vienna, Austria, hatima ya mazungumzo hayo mpaka sasa haitabiriki,
Msimamo huo wa Iran unaashiria vikwazo vilivyopo ambavyo huenda vikakwamisha kupatikana mkataba wa kihistoria kufikia tarehe ya mwisho ya kufikia muafaka hapo Novemba 24. Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani John Kerry amekataa kubashiri matokeo ya mazungumzo hayo ambapo wajumbe kutoka Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani yakiwemo Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, China na Urusi, watajaribu kuumaliza mgogoro uliodumu miaka 12 kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na kuondosha hofu ya kutokea vita vipya Mashariki ya Kati.
Iran imekuwa ikipinga kujadili mambo yasiyousiana na mgogoro wa nyuklia ambayo yamekuwa yakigusiwa na nchi za magharibi, mambo hayo ni pamoja na uwezo wa kijeshi na nguvu za makombora ya Iran ambayo inaonekana kuwa ni tishio kwa nchi zinaohisi kuwa zinauadui na Jamhuri ya kiislamu ya Iran.
Iran imekuwa ikisisitiza kuwa haikukubali kufanya mazungumzo na mataifa ya magharibi kwa sababu ya kuelemewana vikwazo, bali imekubali ili kuielezea dunia kuwa haina nia ya kutengeneza makombola ya maangamizi kama Marekani, Israel na washirika wao wanavyodai.
Iran inasisitiza kuwa inauwezo mkubwa wa kujihami na kukabiliana na maadui zake bila ya kuhitajia makombora ya nyuklia.
Makubaliano haya yakifikia muafaka itakuwa ni hatua ya ushindi kwa serikali ya Obama, kwani ili ahidi kumaliza mgogoro wa nyuklia ya Iran kwa njia ya mazungumzo na amani.
19 Novemba 2014 - 09:29
Msimbo wa Habari: 652338
Jamhuri ya kiisalamu ya Iran imesema itapinga shinikizo lolote la mataifa ya magharibi litakalo lenga kuifanya ikubali masuala magumu na yasiyokubalika katika mazungumzo kuhusu mpango wake wa nyuklia.