Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, ameelezea upinzani wa nchi yake dhidi ya juhudi zozote alizodai zinahujumu mchakato wa uchaguzi wa Israel, huku akisema Marekani inatarajia kutakuwa na njia ya kuendeleza mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati na kuondoa wasiwasi wa Wapalestina. Mkutano wa Kerry wa hapo jana uliwajumuisha mkuu wa ujumbe wa wapatanishi wa Palestina, Saeeb Erakat, na mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Nabil el-Arabi. Kabla ya hapo, Kerry alikuwa amekutana juzi Jumatatu na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, mjini Rome, ambaye alielezea upinzani mkali dhidi ya pendekezo la Palestina na Israel kutaka Umoja wa Mataifa uipe Israel muda na ratiba ya kupatikana kwa suluhisho la mataifa mawili, ikiwemo Israel kuondoa wanajeshi wake kwenye ardhi inayoikalia kwa nguvu. Baadaye, Kerry alikutana na mawaziri wenzake wa mambo ya nje wa Uingereza, Ufaransa na Ujerumani.
Marekani inahofu kubwa kuwa ikiwa ombi hilo la Palestina litajadiliwa katika umoja wa mataifa itakuwa ni mwanzo wa taifa la Israel kurudi nyuma, Marekani inaona kwamba tatizo kati ya Israel na Palestina linatakiwa kuisha kwa njia ya mazungumzo na Israel kuendelea kutawaka adhri ilizozichukua kwa nguvu toka kwa wapalestina, kwa upande wa pili wapalestina wengi wanaona kwamba njia pekee ya kuleta amani kati ya Israel na Palestina ni Israel kurudisha ardhi ilizozichukua kwa nguvu kutoka kwa wapalestina.
Marekani inafanya juhudi zake zote kuhakikisha inatetea maslahi ya Israel na kuhakikisha kwamba ardhi zilizochukuliwa kwa nguvu na Israel zinabaki kuwa mali ya Israel, mukabala na hilo Jamhuri ya kiislamu ya Iran inafanya juhudi zake zote kuhakikisha kwamba Palestina na wote walionyang’anywa ardhi zao na Israel wanzrudisha ardhi zao kwa nguvu na kuitoa Israel katika ardhi zao.