-
Wanazuoni wa Kiislamu watoa fatwa; Mataifa ya Kiislamu yaunge mkono Muqawama wa Palestina
Umoja wa Kimataifa wa Wanazuoni wa Kiislamu (IUMS) umetoa fatwa (agizo la kidini) ukizitaka nchi za Kiislamu kutoa msaada wa haraka wa kijeshi, kifedha na silaha kwa mrengo wa Muqawama wa Palestina, ili kukabiliana na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala katili wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
Safari ya Netanyahu nchini Hungary na kupuuzwa agizo la ICC la kumkamata mhalifu huyo
Afisa mmoja mwandamizi wa serikali ya Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orbán ametangaza kuwa nchi hiyo inajitoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC. Tangazo hilo limetolewa saa chache baada ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu kuwasili mjini Budapest.
-
UN: Israel imegeuza theluthi mbili za ardhi ya Ghaza kuwa eneo lisiloruhusiwa kufika
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imetangaza kuwa, hivi sasa utawala wa Kizayuni wa Israel umewawekea vizuizi Wapalestina vya kutoruhusiwa kufika kwenye takriban theluthi mbili ya eneo la Ukanda wa Ghaza, ama kwa kuyatangaza maeneo makubwa kadhaa ya ukanda huo kuwa ni marufuku kufika au kutoa amri ya kuwalazimisha wananchi hao kuyahama makazi yao.
-
Mkuu wa UNRWA alaani mashambulizi ya Israel dhidi ya majengo ya Umoja wa Mataifa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi wa Kipalestina limelaani vikali mashambulizi ya Israel dhidi ya majengo ya taasisi hiyo huko Gaza.
-
Yemen yalishambulia kwa droni eneo la kijeshi la Israel, Tel Aviv, yatungua droni ya US Sa'daa
Vikosi vya Ulinzi vya Yemen (YAF) vimefanya operesheni ya kijeshi kulenga eneo la jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji wa Yafa kwa kutumia ndege isiyo na rubani ya Yaffa iliyotengenezwa ndani ya Yemen, na kuiangusha pia ndege isiyo na rubani ya Marekani aina ya Giant Shark F360 katika Mkoa wa Sa'daa.
-
Mufti wa Oman akosoa vikali kimya kinachoonyeshwa mbele ya jinai za Israel dhidi ya Ghaza
Mufti Mkuu wa Oman, Sheikh Ahmed al-Khalili, amekosoa vikali kimya kinachoonyeshwa mbele ya jinai za kinyama zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Ghaza.
-
Al Houthi: Marekani imeshindwa katika malengo yake dhidi ya Yemen/ Al Bukhaiti: Hakuna haja ya kuzungumza na Marekani
Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ameashiria jinai za utawala wa Kizayuni kwa kushirikiana na Marekani katika eneo na kusisitiza kuwa mataifa ya Magharibi hayapasi kunyamaza kimya mkabala wa hali ya mambo ya sasa ya Palestina.
-
Hamas: Takriban watoto 19,000 wameuawa shahidi huko Ghaza
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imetangaza kuwa, takriban watoto 19,000 wameshauawa shahidi huko Ghaza na takriban watoto 39,000 wamepoteza kwa uchache mzazi mmoja au wote wawili.
-
Rais wa Iran amfuta kazi Makamu wake kwa 'safari ya ubadhirifu'
Rais Masoud Pezeshkian amempiga kalamu nyekundu Makamu wake katika Masuala ya Bunge kufuatia safari ya kibinafsi ya mwanasiasa huyo wakati wa sherehe za mwaka mpya wa Kiirani (Nowruz), iliyojaa ubadhirifu.
-
Semina ya Mubaghilina wa Mkoa wa Kagera - Wilaya ya Muleba - Tanzania
Kauli mbio yetu ni: Kama Mubalighina ni kuhakikisha malengo ya Mtume (s.a.w.w) yanatimia kwa njia safi ya kuleta umoja, upendo na amani.
-
Habari Pichani | Huduma za Tiba ya Macho Bure Chini ya Taasisi ya Bilal Muslim Mission Tanzania
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA- Ushirikiano Mwema baina ya Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Wadau Wa Maendeleo waendelea kuleta tija na hatimae Wagonjwa Wafurika kwa ajili ya Huduma za Tiba ya Macho Bure chini ya Taasisi ya Bilal Muslim Tanzania, ndani ya Tanga - Tanzania. Na kazi hii ya utoaji wa huduma hii inaendelea mpaka Siku ya Jumatatu. Picha hizi ni kwa hisani ya Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kwakivesa, Handeni, Tanga, ndugu Habib Mbota (Moja kwa Moja), anaye ratibu utoaji wa huduma hii kwa wakazi wa Mkoa wa Tanga.
-
Habari Pichani | Mashindano ya Qur'an Tukufu katika kuhuisha Utajo wa Qur'an Tukufu, Dodoma - Tanzania
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Sambamba na Mwezi Mtukufu wa Ramadhan (1446 AH) Dar-ul-Muslimeen ilipata fursa adhimu ya kufanya Mashindano ya Qur'an Tukufu katika kipengele cha kuhifadhi (Hifdh) kwa Wanafunzi wa Dar-ul-Muslimeen Nursery, Shule ya Msingi na Sekondari. Mashindano haya hufanywa kwa kila mwaka. Na Washindi na Washiriki wote walifanikiwa kupokea zawadi, Al-Hamdulillah.
-
Fiqh Na Hukumu Zake:
Namna ya Kutoharisha vitu vilivyo najisika kwa kutumia Maji
Anuani ya makala yetu inasema: "Kwa kutumia Maji" kwa kuwa maji ndio yaliyochukua nafasi kubwa katika kutoharisha vilivyonajisika kuliko vingine vyote vyenye kutoharisha.Tutamia herufi (S) kuashiria swali na herufi (J) kuashiria jibu lake.
-
Majukumu ya Mwanalimu na Mwanafunzi (1)
Majukumu ya Mwalimu yamegawanyika katika sehemu kuu tatu :- Majukumu yake binafsi, majukumu juu ya wanafunzi wake, na majukumu yake akiwa darasani.
-
Video + Mwanachuoni huyu wa Kisunni anasema "Sisi tunajikurubisha kwa Allah kwa kumpenda Hassan, na Hussein, na Fatima na Ali"
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Mwanachuoni huyu wa Kisunni anasema "Sisi tunajikurubisha kwa Allah kwa kumpenda Hassan, na Hussein, na Fatima na Ali. Ama Ali bin Abi Talib (a.s) kumzungumzia kunahitajia ratiba kamili. Lakini inanitosha kumzungumzia Ali (a.s) kwa maneno aliyoyasema Mtume (s.a.w.w) kumhusu kwamba: " Je, huridhii wewe kuwa na daraja kwangu mimi kama ile aliyokuwa nayo Harun kwa Mussa (a.s), ispokuwa hakuna Nabii baada yangu?!. Kisha akasema Mtume (s.a.w.w) kuhusu Ali (a.s) siku ya vita vya Khaibar: "Hakika kesho nitampa Bendera hii mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda.Mwenyezi Mungu ataileta ushindi wa Khaibar kupitia (mtu huyu).Yeye kamwe hakimbii vitani."".
-
Habari Pichani | Waumini wa Kiislamu, Wafuasi wa Ahlul-Bayt (as) nchini Kenya wakisherehekea Siku Kuu ya Eid - al-Fitr
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Waumini wa Kiislamu, Wafuasi wa Ahlul-Bayt (as) wakiwa katika Hali ya kusherehekea Siku Kuu ya Eid - al-Fitr Nchini Kenya.
-
Mazungumzo ya Biashara Kati ya Kenya na Iran
Mazungumzo makubwa na muhimu ya Iran na Kenya kuhusu kuimarisha uhusiano wa kibiashara baina ya nchi mbili.
-
Tunajifunza nini baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan?
Aliyekuwa akifanya Ibada za Usiku ndani ya Ramadhani na mwendo wake ukabadilika na tabia zake kuwa nzuri ndani ya Ramadhan, basi aendelee kuwa na tabia nzuri hivyo hivyo hata baada ya Ramadhan. Na hii ni sehemu ya wito na funzo zuri toka kwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w).