-
Kongamano la Maridhiano na Amani la (JMAT) – Kata ya Vijibweni, Wilaya ya Kigamboni, Mkoa wa Dar-es-Salaam, Tanzania +Picha
Viongozi wa JMAT walisisitiza kwamba maridhiano na mshikamano ni msingi wa maendeleo ya taifa, huku wakihimiza jamii kuendeleza mazungumzo ya upendo, heshima na mshikamano.
-
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Dar-ul-Muslimeen Waadhimisha Arubaini ya Imam Hussein (a.s) +Picha
Mkusanyiko huu ulilenga kukuza mapenzi kwa Ahlul-Bayt (a.s.) ndani ya nyoyo za watoto na kuwajengea mafunzo ya kupinga dhulma na kusimama kidete katika haki, kama linavyofundisha tukio la Karbala.
-
(Radi amali) Mwitikio wa Maduro kwa Kupelekwa kwa Manowari za Marekani Venezuela
Rais wa Venezuela ameikosoa hatua ya Marekani ya kupeleka manowari tatu za kivita karibu na pwani ya nchi yake, akitaja kitendo hicho kuwa ni “uvamizi wa kigaidi wa kijeshi, usio halali na kinyume cha sheria.”
-
Kikao cha Kielimu cha wanafunzi wa Madrasa ya Mabinti chaadhimisha kumbukumbu ya shahada ya Imam Hasan al-Mujtaba (a.s)
Katika kikao hicho, mada kuu iliyojadiliwa ilikuwa: Athari na maana ya Amani ya Imam Hasan (a.s) – wanafunzi walitathmini hali ya kisiasa ya zama zake na hekima iliyopelekea kufanya mapatano ya amani na Mu’awiya, pamoja na athari zake kwa kulinda dini ya Uislamu.
-
Majlisi ya Kumbukumbu ya Shahada ya Imam Ali bin Musa al-Ridha (a.s) yafanyika sambamba na Qur’ani na Dua ya Nudba +Picha
Sheikh Dkt. Saleh Maulid kuhusiana na Nafasi ya kielimu ya Imam Ridha (a.s) alibainisha namna Imam alivyoshiriki katika mijadala ya kielimu na kihistoria katika zama za Abbasiyya, na mchango wake mkubwa katika kuimarisha hoja za Kiislamu mbele ya wajuzi na wanazuoni wa nyakati zake".
-
Chuo cha Al-Mustafa (s) Dar-es-salaam - Tanzania chaendesha mtihani wa kila wiki kwa wanafunzi wake +Picha
Kwa mujibu wa viongozi wa chuo, mtihani wa kila wiki ni chombo muhimu cha kielimu kinachosaidia kufuatilia maendeleo ya wanafunzi, kubaini changamoto wanazokabiliana nazo, na kuweka mikakati ya kuboresha zaidi mbinu za ufundishaji na ujifunzaji.
-
Mazishi ya Sheikh Iddi Yasin yafanyika Temeke sambamba na Maadhimisho ya Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) + (Picha +Video)
Sheikh H.Jalala alisema: “Nimemsoma Mtume Muhammad (s.a.w.w), tabia na maadili yake. Mtume alikuwa mtu mwenye uwezo wa kuishi na kila mtu katika jamii. Sheikh Iddi Yasin alijipamba kwa tabia hii ya Mtume, na jamii imemtambua hivyo. Huenda kwa sababu ya kufanana huku, Mwenyezi Mungu amemchukua katika siku hizi za kumbukumbu ya kifo cha Mtume (s.a.w.w).”
-
Wanafunzi Wajadili Maisha na Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) Katika Kikao cha Kielimu - Hawzat ya Imam Zaynul Aabidin (a.s) - Burundi + Burundi
washiriki walipata nafasi ya kusikiliza, kuuliza maswali na kujadiliana kuhusu masuala muhimu yanayohusu maisha na nafasi ya Mtume (s.a.w.w) katika kuongoza Umma wa Kiislamu.
-
Wanafunzi na Walimu wa Jamiat Al-Mustafa (s) Wamuombea Dua ya Maghfira Marhumu, Sheikh Yasin Idi Bashemera kwa Kisomo cha Surat Yasin +Picha
Qur'an Tukufu: "Mwenyezi Mungu huzichukua nafsi wakati wa kufa kwake, na ambazo hazijafa katika usingizi wake…"
-
"Vipi tutafurahika na Mtume katutoka?!" – Nauha ya Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) | Jamiat Al-Mustafa (s) - Dar es Salaam - Tanzania +Video
Nauha hii ni sehemu ya jitihada za kuenzi kumbukumbu ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kuwakumbusha Waislamu dunia nzima juu ya nafasi yake tukufu, mchango wake mkubwa katika maisha ya Umma, na mapenzi ya dhati ya wafuasi wake kwake.
-
Araqchi: Taliban Haijaheshimu Haki za Waislamu wa Kishia wa Afghanistan
Ikumbukwe kuwa, baada ya kurejea madarakani, Taliban ilifuta rasmi Sheria ya Hali ya Kiraia ya Waislamu wa Kishia, na kuondoa vitabu vyote vya Fiqh ya Ja’fari kutoka vyuo vikuu, shule na maktaba za serikali. Kundi hilo limekuwa likisisitiza kwamba sheria za Afghanistan lazima zitekelezwe kwa mujibu wa Fiqh ya Kihanifi pekee.
-
Madrasa ya Wasichana ya Hazrat Zainab (sa) Kigamboni - Yaadhimisha Arubaini ya Imam Hussein (a.s) kwa Majlisi Maalum ya Maombolezo
Kikao hicho kilipambwa kwa kisomo cha Qur’an Tukufu na mashairi ya maombolezo (marsiya), ambapo walimu na wanafunzi walishiriki kwa unyenyekevu na hisia za heshima kwa mashahidi wa Karbala.
-
Kikao Maalum cha Uchambuzi wa Masomo ya Qur’an Tukufu Chafanyika Madrasa ya Wasichana ya Hazrat Zainab (sa) - Kigamboni, Dar-es-salaam
Katika kikao hicho, walimu mbalimbali walitoa maoni kuhusu mbinu bora za kufundishia na kuhimiza nidhamu ya kielimu, huku wanafunzi nao wakipewa nafasi ya kueleza changamoto wanazokutana nazo.
-
Chuo cha Al-Mustafa(s) - Mbezi Beach, Dar-es-salaam Chafanya Vipimo vya Afya kwa Wanafunzi wa Kiume +Picha
Lengo kuu la zoezi hili lilikuwa ni kugundua mapema changamoto za kiafya zinazoweza kuathiri masomo na maisha ya kila siku ya wanafunzi, pamoja na kuhamasisha tabia za afya njema.
-
Habari Pichani | Mdahalo wa Kitaifa ulioratibiwa na Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) kwa kushirikiana na Global Peace Foundation
Akizungumza katika mdahalo huo, Sheikh Dkt. Al-Hadi Mussa Salum, Mwenyekiti wa JMAT, alisema: "Uchaguzi ni fursa ya kuonyesha uzalendo na kuchagua viongozi kwa njia ya amani".
-
JMAT TAIFA:
Mdahalo wa Viongozi wa Dini na Siasa: Wito wa Kudumisha Amani na Demokrasia Safi kuelekea Uchaguzi Mkuu
Sheikh Dkt. Al-Hadi Mussa Salum: "Amani na Utulivu nchini ni msingi wa maendeleo ya Taifa na Ustawi wa kila Mtanzania".
-
Miaka 10 ya Uongozi wa Mufti wa Tanzania Dr.Abubakar Zubair: Historia ya Mafanikio na Maboresho Makubwa
Miradi mikubwa yenye thamani ya mabilioni imetekelezwa katika mikoa mbalimbali, huku maboresho ya kiutawala na ya kimuundo yakifanikishwa, ikiwemo kuanzishwa kwa Ofisi ya Mufti, JUWAKITA na JUVIKIBA, pamoja na mabadiliko ya Katiba ya BAKWATA ili kuendana na mahitaji ya sasa.
-
Sauti za Mshikamano wa Mexico na Palestina katika Barabara za Jiji Kuu
Maelfu ya wananchi mjini Mexico City waliungana katika maandamano makubwa yaliyopewa jina “Mexico kwa Palestina”, wakilaani jinai za utawala wa Kizayuni na uungaji mkono wa Marekani, huku wakidai kusitishwa kwa mauaji ya kimbari Gaza na kutumwa haraka kwa misaada ya kibinadamu.
-
Matembezi ya Kumbukizi ya Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) Kuandaliwa Dar es Salaam kupitia Hawzat Imam Swadiq (as)
Tukio hili linatarajiwa kuwa jukwaa la mshikamano wa Kiislamu na nafasi ya kumuenzi Mtume wa Rehema (s.a.w.w) kwa ibada, dua na kuonesha mapenzi yetu kwake.
-
Waumini wa Wilaya ya Siha waadhimisha Arubaini ya Imam Hussein (as) na Mashahidi wa Karbala kwa Ibada na Uchangiaji Damu +Picha
Waumini walipata nafasi ya kujikumbusha ujumbe wa Arubaini - msisitizo wa upendo, kujitolea na mshikamano wa Kiislamu -sambamba na kushiriki kwa vitendo katika kuokoa maisha kupitia uchangiaji damu.
-
Ziara ya kundi la Wanafunzi wa Jāmi‘at al-Mustafā al-‘Ālamiyyah katika Taasisi ya Utafiti ya Dhūriyyah Nabawiyyah +Picha
Wakati wa ziara hiyo, walipata fursa ya kujionea kwa karibu shughuli za kielimu na utafiti zinazofanywa na taasisi hiyo, hususan katika uwanja wa nasaba za Maimamu na Masayyid.
-
Ridhwan Kikwete: Miongozo ya Kima cha Chini Cha Mshahara Kusainiwa Hivi Karibuni
Serikali imedhamiria kuhakikisha wafanyakazi wa sekta binafsi wananufaika na viwango vipya vya mishahara, hatua inayotarajiwa kuboresha hali ya maisha na kulinda heshima ya kazi nchini.
-
Israel Inakusudia Kutuma Misaada ya Dharura kwa Sudan Kusini
Wakati utawala wa Israel umefunga vivuko vyote vya Gaza na kuzuia kuingia kwa misaada ya kibinadamu, Wizara ya Mambo ya Nje ya utawala huu imetangaza kutuma misaada ya dharura kwa Sudan Kusini.
-
Mwenyekiti wa JMAT-TAIFA Ashiriki Harusi ya Mtoto wa Rais wa Zanzibar +Picha
Aidha, Sheikh Dkt.Alhad Mussa Salum, ametumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa niaba ya JMAT na ambapo alisema: "Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA) inatoa pongezi za dhati kwa familia ya Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na kuwaombea wanandoa wapya maisha yenye upendo, baraka na amani ya kudumu".
-
Mwitikio wa Al-Azhar kwa Udanganyifu wa Kuundwa kwa "Israeli Kubwa"
Taasisi ya Al-Azhar ya Misri imelaani matamko ya Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni kuhusu "Israeli Kubwa" na kuelezea maneno hayo kama "udanganyifu" na "hotuba za uchochezi".
-
Walimu Wapya Watambulishwa Madrasa ya Fatima Zahraa (s.a), Waumini Wajumuika na Sayyid Arif Naqvi katika Sala ya Jamaa
Sheikh Eid aliwapa wanafunzi nasaha kuhusu umuhimu wa kujitahidi katika masomo yao na kusisitiza nafasi ya elimu ya dini katika kujenga jamii yenye maadili mema.
-
Majlisi ya Arubaini ya Imam Hussein (as) - Arusha Tanzania +Picha
Khatibu wa Majlis (Shekh Ridhwa Dosa), aliangazia Falsafa ya Maombolezo ya Arubaini ya Imam Hussein (as) Fadhila za kumzuru Mjukuu wa Mtume (saww), Hussein bin Ali bin Abi Talib (as).
-
Hawza ya Sayansi ya Kiislamu ya Imam Ridha (a.s) Ikwiriri - Rufiji, Tanzania yafanya Maadhimisho ya Arubaini ya Imam Hussein(a.s) + Picha
Majlisi hii imehudhuriwa na waumini wengi kutoka maeneo mbalimbali, jambo lililoonesha wazi upendo, uaminifu na utiifu wao kwa mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), Imam Hussein (a.s).
-
Mitihani ya Kila Wiki - Chuo Kikuu cha Al-Mustafa(s), Dar es Salaam - Tanzania
Mchakato huu umefanyika chini ya usimamizi makini wa walimu na uongozi wa chuo ili kuhakikisha haki, uadilifu wa kielimu na nidhamu ya kimasomo vinazingatiwa ipasavyo.
-
Muendelezo wa Majalisi za Arubaini ya Imam Hussein (a.s) - Arusha, Tanzania +Picha
Majalisi hizi pia zimekuwa fursa ya kuonesha mshikamano wa Waislamu wa Tanzania na ulimwengu mzima katika kuhuisha kumbukumbu ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s), tukio linalojulikana kwa kuwakutanisha mamilioni ya waumini katika mji wa Karbala kila mwaka.