Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (AS) - Abna - Vyanzo vya Habari vimeripoti kuhusu mashambulizi makubwa ya anga ya ndege za Kijeshi za Israel katika maeneo tofauti ya Ukanda wa Gaza.
Kwa mujibu wa ripoti hii, raia 131 wa Palestina wameuawa Shahidi katika duru hii ya mashambulizi ya anga ya Israel katika Ukanda wa Gaza, na wengi wa Mashahidi hao walikuwa Wanawake na Watoto.
Jeshi la Israel limeeleza kuwa, lengo la mashambulizi hayo ya anga ni kufikia malengo ya vita yaliyowekwa na safu za kisiasa ikiwemo kuachiliwa huru mateka wote wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.
Kuhusiana na kuanza tena mashambulizi katika Ukanda wa Gaza, Waziri wa Ulinzi wa Israel Yisrael Katz alisema: "Kwa sababu ya Hamas kukataa kuwaachilia mateka na tishio la kuwadhuru wanajeshi wa Israel na jamii za Israel, tumeamua kurejea kwenye vita huko Gaza usiku huu."
Aliendelea: "Ikiwa Hamas haitawaachilia mateka wote, milango ya kuzimu itafunguka huko Gaza na wauaji na wavamizi wa Hamas watakutana na jeshi la Israeli na vikosi ambavyo hawajawahi kujua hapo awali."
Waziri wa Ulinzi wa Israel amesisitiza kuwa: Hatutaacha kupigana hadi watekwaji nyara warudi nyumbani na kufikia malengo yote ya vita.
Ikulu ya Marekani pia ilitangaza kuwa, utawala wa Kizayuni ulishauriana na Washington kabla ya kufanya mashambulizi katika Ukanda wa Gaza.
Your Comment