5 Juni 2026 - 21:00
ABNA Yampongeza Sheikh Prof. Alhad Mussa Salum kwa Uongozi Wake wa Kuimarisha Amani na Maridhiano Nchini Tanzania

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt News Agency (ABNA) limetoa pongezi kwa Sheikh Prof. Alhad Mussa Salum kwa mchango wake katika kukuza maridhiano ya kijamii, kuimarisha umoja wa kitaifa na kudumisha amani, akiwa kielelezo cha uongozi wenye hekima na busara, katika siku muhimu ya kuzaliwa kwake.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- tunatoa salamu za pongezi za dhati kwa Sheikh Prof. Alhad Mussa Salum, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA).

Sheikh Prof. Alhad Mussa Salum anathaminiwa kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha maridhiano ya kijamii, umoja wa kitaifa na kudumisha amani, akiwa ni kielelezo cha uongozi wenye hekima, busara na uzalendo unaozingatia maslahi mapana ya jamii.

Kupitia jitihada zake, amekuwa mstari wa mbele katika kuhimiza maelewano, heshima na mshikamano wa kijamii, jambo linalomfanya kuheshimika ndani na nje ya nchi ya Tanzania.

Kwa heshima hiyo, ABNA inamtakia Siku Njema ya Kuzaliwa, ikiomba kwa Mwenyezi Mungu amjaalie afya njema, umri mrefu wenye baraka, hekima na kheri kwa Taifa na Ulimwengu wa Amani, na aendelee daima kuwa chachu ya amani na umoja katika jamii.

Happy Birthday Sheikh Prof. Alhad Mussa Salum .

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha