Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Sayyid Ammar al-Hakim na Ayatullah Ramadhani Wajadili Uimara wa Iran na Mchakato wa Kuunda Serikali Mpya Iraq
Mwenyekiti wa Muungano wa Nguvu za Kitaifa wa Iraq, Sayyid Ammar al-Hakim, amekutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (as), Ayatollah Reza Ramezani, katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad, ambapo walijadili maendeleo ya kisiasa nchini Iraq na hali ya eneo la Mashariki ya Kati.
Katika mkutano huo, Sayyid Ammar al-Hakim alitoa salamu za rambirambi kufuatia kile alichokitaja kuwa ni kuuawa shahidi kwa Ayatollah al-Udhma Imam Khamenei (Quddisa Sirruh), akieleza kuwa tukio hilo limewaathiri kwa huzuni wapenzi na wafuasi wa Ahlul-Bayt (as).
Aidha, alieleza namna Iraq ilivyofanikiwa kutoka katika mkwamo wa kisiasa na kuendesha mchakato wa uhamishaji wa madaraka kwa amani kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo, akisisitiza umuhimu wa kuheshimu misingi ya kikatiba katika kujenga utulivu wa kisiasa.
Kwa upande wake, Ayatullah Ridha Ramadhani alisifu ustahimilivu na mshikamano wa wananchi wa Iran katika kukabiliana na changamoto mbalimbali. Pia alielezea hatua ya Baraza la Wataalamu wa Uongozi (Majlis-e Khobregan) ya kumchagua na kumtangaza kwa haraka Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei, wakati wa mazingira magumu ya vita, kuwa ilikuwa uamuzi wa busara na wenye kuimarisha utulivu.
Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa uwepo wa kiongozi huyo, pamoja na sifa zake za uchamungu, elimu ya fiqhi na uadilifu, ni neema kubwa kwa Umma wa Kiislamu.
Your Comment