22 Juni 2026 - 19:06
Makamu wa Rais wa Iran: Tuliyaonya Mataifa Jirani Kuhusu Silaha za Marekani na Tutaendelea Kulinda Maslahi Yetu

Makamu wa Rais wa Iran, Mohammad Reza Aref, amesema Tehran iliziarifu rasmi nchi jirani kuwa silaha zozote za Marekani zitakazoingia Iran kupitia Ardhi zao, Ardhi hizo zitachukuliwa kuwa sehemu ya uwanja halali wa kujilinda wa Iran.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mohammad Reza Aref, amesema kuwa serikali ya Iran iliziarifu rasmi nchi jirani wakati wa mazungumzo kwamba ikiwa silaha za Marekani zitaingia Iran kupitia maeneo yao, hata kama itakuwa kwa makosa, maeneo hayo yatachukuliwa kuwa sehemu halali ya hatua za kujihami za Iran.

Aref amesema msimamo huo unatokana na haki ya Iran ya kulinda usalama na mamlaka yake ya kitaifa dhidi ya vitisho vya nje.

Aidha, amesisitiza kuwa Iran ina uwezo wa kuvuka changamoto kama ilivyofanya wakati wa vita vya miaka minane, akieleza kuwa taifa hilo limejijengea uwezo wa kustahimili mashinikizo na migogoro mbalimbali.

Makamu huyo wa Rais pia amesema Iran inajiona kuwa "ndugu mkubwa" katika eneo la Mashariki ya Kati, akieleza kuwa inalenga kusaidia kufanikisha malengo na maslahi ya mataifa mengine ya eneo hilo kwa mujibu wa mtazamo wa Tehran.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha