3 Julai 2026 - 11:17
Qalibaf: Kulipiza kisasi kwa Kiongozi wa Mapinduzi ni kuwaweka huru Waislamu kutoka katika dhulma za Marekani na utawala wa Kizayuni

Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amesema kuwa njia ya kuenzi urithi wa Kiongozi Shahidi wa Umma wa Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ni kuendelea kuiunga mkono Kambi ya Muqawama, hususan Lebanon, na kupambana na ubeberu wa Marekani na utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, amesema kuwa kisasi cha kweli kwa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ni kuwaweka huru Waislamu kutokana na dhulma za Marekani na utawala wa Kizayuni.

Qalibaf aliyasema hayo alipokutana na ujumbe wa Amal Movement kutoka Lebanon, ambapo alisisitiza kwamba uaminifu kwa njia na misingi ya kiongozi huyo shahidi unahitaji kuendelea kuiunga mkono Kambi ya Muqawama, hususan nchini Lebanon, pamoja na kupambana na ubeberu wa Marekani na utawala wa Kizayuni.

Aidha, Spika huyo wa Bunge la Iran alieleza umuhimu wa nafasi ya Spika wa Bunge la Lebanon, Nabih Berri, akisisitiza kuwa Iran inaunga mkono uamuzi wowote atakaouchukua kwa kuzingatia maslahi ya taifa la Lebanon na kwa makubaliano ya kitaifa.

Kwa upande wake, kiongozi wa Harakati ya Amal, Khalil Hamdan, aliwasilisha salamu za rambirambi kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kufuatia kuaga dunia kwa Kiongozi Shahidi, na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza na kuwatambulisha vizazi vijavyo sifa, mchango na misimamo ya kiongozi huyo katika kuutetea Umma wa Kiislamu na Muqawama.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha