7 Julai 2026 - 15:44
Jenerali Qaani: Mazishi ya Sayyid Ali Khamenei Nchini Iraq Yataimarisha Umoja Dhidi ya Fitna na Kuhuisha Wito wa Haki

Kamanda wa Kikosi cha Quds amesema marasimu ya mazishi ya Sayyid Ali Khamenei nchini Iraq yataonyesha mshikamano wa wananchi wa Iraq na Iran, na kuimarisha msimamo wa pamoja dhidi ya fitna na migawanyiko.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) – ABNA – Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Jenerali Ismail Qaani, amesema kuwa marasimu ya mazishi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Shahidi Sayyid Ali Khamenei, yatakayofanyika nchini Iraq yataimarisha mshikamano kati ya mataifa ya Iraq na Iran na kuonyesha msimamo wao wa pamoja dhidi ya fitna na migawanyiko.

Katika ujumbe wake, Jenerali Qaani amesema maandalizi ya serikali na wananchi wa Iraq ya kuandaa tukio hilo la kihistoria yanaakisi uhusiano wa karibu wa kiroho kati ya wananchi wa nchi hizo mbili.

Aidha, amesema kuwa uungaji mkono wa Sayyid Ali Khamenei kwa wananchi wa Iraq na nafasi ya Marjaiyyah katika kukabiliana na ugaidi uliwezesha ushirikiano wa karibu kati ya Shahidi Qassem Soleimani, wapiganaji wa Iraq na vikosi vya kujitolea katika mapambano dhidi ya kundi la Daesh.

Ameongeza kuwa marasimu ya mazishi ya Sayyid Ali Khamenei nchini Iraq, kama ilivyokuwa kwa mazishi ya Shahidi Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandis, yatazidi kuimarisha mshikamano wa wananchi wa Iraq na Iran na kuonyesha azma yao ya kusimama pamoja dhidi ya migawanyiko na changamoto zinazolikabili eneo hilo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha