9 Julai 2026 - 14:33
Iran Yatangaza Kushambulia Malengo ya Kijeshi ya Marekani Nchini Qatar

Iran imetangaza kuwa imefanya mashambulizi dhidi ya malengo ya kijeshi ya Marekani yaliyoko nchini Qatar ikijibu mashambulizi ya Marekani Dhidi yake na katika hatua inayoashiria kuongezeka kwa mvutano wa kijeshi kati ya Tehran na Washington.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa imefanya mashambulizi dhidi ya malengo ya kijeshi ya Marekani nchini Qatar, ikiwa ni sehemu ya majibu yake kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni ya Marekani dhidi ya maeneo ya Kusini mwa Iran. 

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari vya Iran, mashambulizi hayo yalilenga miundombinu ya kijeshi ya Marekani iliyopo Qatar. Wakati huohuo, mamlaka za Qatar na Marekani zinaendelea kufuatilia hali hiyo, huku taarifa kuhusu kiwango cha uharibifu au majeruhi zikiendelea kukusanywa.

Tukio hilo linaongeza wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa mvutano wa kijeshi katika eneo la Ghuba, wakati juhudi za kidiplomasia za kupunguza mzozo kati ya Iran na Marekani zikiendelea kukabiliwa na changamoto.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha