Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei, ametoa ujumbe muhimu kwa wananchi waaminifu na wapambanaji wa Iraq, akipongeza maandamano makubwa na ya kihistoria ya mazishi ya mwili mtakatifu wa kiongozi shahidi wa Muqawama katika maeneo matakatifu nchini humo.
Katika ujumbe wake, Ayatollah Sayyid Mojtaba Khamenei amesisitiza kuwa mazishi hayo ya mamilioni ya watu, yaliyokuwa ya kipekee na yasiyo na mfano, yameonesha kwa uwazi mshikamano, undugu na umoja wa misimamo baina ya wananchi wa Iraq na Iran.
Amesema kuwa tukio hilo kubwa limeonesha kwamba uhusiano wa wananchi wa mataifa hayo mawili hauwezi kuvunjwa na njama za maadui, akibainisha kuwa Marekani, inayotajwa kuwa “Shetani Mkuu”, sasa imeelewa kuwa kuendelea kuwepo kwake katika eneo hilo kwa urahisi na kwa mtazamo wa kutawala ni ndoto isiyowezekana.
Kiongozi huyo ameeleza kuwa ushiriki mkubwa wa wananchi katika kuaga kwao kwa kihistoria kiongozi huyo shahidi umeweza kuzima njama za maadui za kuchochea mifarakano na kuwagawa wananchi.
Aidha, amesema kuwa ushiriki wa makumi ya mamilioni ya wananchi nchini Iran na Iraq, kwa ajili ya kushiriki katika mazishi na kumuaga Imam huyo mpambanaji na shahidi — Mwenyezi Mungu aiinue daraja yake — umefungua ukurasa mpya wa mwamko na nafasi ya wananchi katika kubadilisha mizani iliyopangwa na madola ya kiburi duniani.
Amesisitiza kuwa tukio hilo kubwa la kihistoria limeonesha nguvu ya umoja wa wananchi, mshikamano wa mataifa ya eneo hili na uwezo wao wa kushiriki katika kuunda mustakabali mpya wa kisiasa na kiusalama, kinyume na mipango ya madola yenye kutaka kulazimisha matakwa yao juu ya watu wa eneo hilo.
Maoni yako