19 Julai 2026 - 21:14
Araghchi: Iran Iliingia Katika Mazungumzo Ili Kuthibitisha Kuwa Marekani na Israel Hawawezi Kujadiliana kwa Uaminifu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema kuwa Iran iliingia katika mazungumzo baada ya kutumia njia zote za kidiplomasia, ili kuthibitisha kwamba tatizo halikutokana na kutokuwepo kwa mazungumzo.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi amesema kuwa hatimaye uamuzi ulifikiwa wa kuingia katika mazungumzo, hasa kwa lengo la kuthibitisha kwamba Iran ilikuwa imetumia kikamilifu njia zote za kidiplomasia.
 
Amesema hatua hiyo ililenga kuhakikisha kwamba baadaye hakuna mtu ambaye angeweza kusema: “Laiti mngeingia katika mazungumzo, vita visingetokea.”
 

Kwa mujibu wa Araqchi, Iran ilitaka kuthibitisha kwa vitendo kwamba ilikuwa tayari kutumia diplomasia, lakini licha ya mazungumzo hayo, njia ya kidiplomasia haikuweza kuzuia kuibuka kwa mzozo na vita baada ya Marekani na washirika wake kuibua tena Mashambulizi dhidi ya Iran.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha