Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– aliyekuwa Waziri Mkuu wa Iraq, Mohammed Shia' al-Sudani, amelaani kwa maneno makali mashambulizi yaliyolenga makao ya vikosi vya Hashd al-Shaabi nchini Iraq, akiyataja kuwa ni ukiukaji wa wazi wa mamlaka ya taifa hilo.
Al-Sudani amesema kuwa mashambulizi hayo ya Saudi Arabia na Marekani yanawakilisha uvunjaji mkubwa wa uhuru wa Iraq, ukiukaji wa sheria za kimataifa pamoja na Mkataba wa Umoja wa Mataifa.
Aidha, amesisitiza kuwa Iraq inahifadhi kikamilifu haki zake halali zinazotambuliwa na sheria za kimataifa, ikiwemo haki ya kulinda mamlaka yake, ardhi yake na wananchi wake dhidi ya vitendo vya uchokozi.
Aliyekuwa Waziri Mkuu huyo ameongeza kuwa kuhujumiwa kwa usalama na utulivu wa Iraq ni jambo lisiloweza kukubalika wala kuvumiliwa, akitoa wito wa kuheshimiwa kwa mamlaka ya taifa hilo na kusitishwa kwa vitendo vinavyohatarisha amani na usalama wa eneo hilo.
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Iraq Alaani Mashambulizi ya Saudi Arabia na Marekani dhidi ya Hashd al-Shaabi
29 Julai 2026 - 21:56
Msimbo wa Habari: 1846720
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Iraq, Mohammed Shia' al-Sudani, amelaani vikali mashambulizi yaliyofanywa na Saudi Arabia na Marekani dhidi ya makao ya Hashd al-Shaabi, akisema ni ukiukaji mkubwa wa mamlaka ya Iraq na sheria za kimataifa.
Maoni yako