Kumetokea mapambano makali na kurushiana silaha baina ya jeshi la Lebanon na magaidi wa Jabhatu Nusra.
Magaidi hao walikuwa wanajaribu kuingia Lebanon kupitia mipaka ya Syria, katika mapambano hayo makali jeshi la Lebanon likishirikiana na jeshi la mpakani la Syria pamoja na askari wa Hizbollah walifanikiwa kuwaangamiza magaidi hao na kuwazuia wasiweze kuingia Lebanon.
Mapambano mengine yalitokea baina ya jeshi la Lebanon na magaidi hao katika mji wa Tarablos, mapambano haya yalisababishwa wakazi wengi wa mji huo, kukimbia makazi yao.
Kitongoji Babul Tabana kilichopo katika mji wa Tarablos kilikuwa moja ya ngome ya magaidi hao, ambapo baada ya mashambulizi mazito na mapambano ya muda mrefu yaliyofanywa na jeshi la Lebanon yalipelekea magaidi hao kurudi nyuma na kuacha vitu vyao vya thamani ikiwemo kiwanda cha silaha.
Ikumbukwe kuwa mnano mwezi Agost mwaka huu, magaidi wa Daesha wakishirikiana na Jabhatu nasr waliteka mji wa Arsal, uliyopo umbali wa kilometa 124 toka mji mkuu wa Lebanon, Beirut, ambapo waliteka askari 3o wa Lebanon na kuwachinja watatu kati yao.
30 Oktoba 2014 - 07:07
News ID: 647885

Kumetokea mapambano makali na kurushiana silaha baina ya jeshi la Lebanon na magaidi wa Jabhatu Nusra.