23 Oktoba 2025 - 18:39
Siri iliyofichuliwa na wafungwa wa Palestina kutoka katika gereza la Israel kuhusiana na wafungwa waliopotea wa Lebanon

Baadhi ya waliokuwa huru wamesema kuwa walikutana na Walebanon waliokuwa wameorodheshwa awali kama waliopotea katika magereza ya Ofer, Nafha, Ramla, na Ashkelon.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Kuachia huru kundi la wafungwa wa Palestina katika makubaliano ya hivi karibuni na Israel, kumeanzisha upya mjadala kuhusu wafungwa wa Lebanon na waliopotea.

Kulingana na ripoti ya Al-Akhbar, baadhi ya wafungwa wa Palestina walioachiwa huru wamesema kuwa walikutana na Walebanon waliokuwa wameorodheshwa awali kama Walebanon waliopotea katika magereza ya Ofer, Nafha, Ramla, na Ashkelon.

Kutokana na kukosekana kwa ufuatiliaji rasmi kutoka Serikali ya Lebanon, familia za wafungwa zimechukua hatua binafsi ili kupitia mawasiliano na wafungwa walioachiwa huru wa Palestina, wapate dalili za hatima ya watoto wao.

Ripoti zinaonyesha kuwa takriban Walebanon 30 bado wako katika magereza ya Israel.

Mfano mmoja ni Ali Tarhini, kijana wa miaka 19, ambaye mama yake alithibitisha kupitia mmoja wa wafungwa wa Palestina walioachiwa huru kuwa yu hai na anateseka kutokana na majeraha aliyopata wakati wa kuwekwa kizuizini.

Vilevile, majina kama Hassan Qashqoush, Hadi na Ali Assaf, na Abdullah Fahda, baada ya muda mrefu bila habari, yamepatikana miongoni mwa wafungwa waliotambuliwa.

Hata hivyo, taasisi rasmi za Lebanon hazijatoa majibu madhubuti.

Kulingana na ripoti, hatua moja ya dhahiri iliyochukuliwa ni kutoa orodha ya wafungwa 16 na waliopotea 65 kutoka kwa Usalama wa Umma, ambayo, kwa kuzingatia ushuhuda mpya, inaongeza uwezekano kwamba baadhi yao bado wapo hai.

Ingawa majina hayo mapya yanatokea kutoka ndani ya magereza ya Israel, kimya rasmi bado kinaendelea kushuhudiwa kutoka Serikali ya Lebanon.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha