8 Desemba 2025 - 13:12
Turki Al-Faisal: Israel ndiyo tishio kuu kwa uthabiti wa eneo hili; si Iran

Chaguo la Nyuklia kwa Riyadh: Al-Faisal, alipoulizwa kuhusu uwezekano wa Saudi Arabia kuendeleza uwezo wa nyuklia, alisema: “Hili ni chaguo ambalo Riyadh inapaswa kulichunguza kwa uzito na kwa umakini mkubwa.”

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-, Abu-Dhabi | Turki Al-Faisal, mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi ya Saudi Arabia, amesema kuwa Israel ndiyo tishio kuu kwa uthabiti wa Mashariki ya Kati, na si Iran.

Akizungumza katika mkutano wa “Mashariki ya Kati na Afrika” uliofanyika mjini Abu Dhabi, Al-Faisal alisisitiza kuwa vitendo na mashambulizi ya mara kwa mara ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon, Gaza na Syria vinaonesha wazi kuwa Israel haijali mchakato wa amani, na kwa hakika ndiyo inayohatarisha usalama wa eneo zima.

Aidha, aliitaja shambulizi dhidi ya wajadiliano wa Hamas huko Doha, wakati walipokuwa wakijadili mapendekezo ya kusitisha mapigano huko Gaza, kuwa ni ishara hatari na ya kuonya, akasema tukio hilo linaonesha wazi kwamba nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba (GCC) zinapaswa kuungana kwa dhati kwa ajili ya kujilinda.

Turki Al-Faisal: Israel ndiyo tishio kuu kwa uthabiti wa eneo hili; si Iran

Chaguo la Nyuklia kwa Riyadh

Al-Faisal, alipoulizwa kuhusu uwezekano wa Saudi Arabia kuendeleza uwezo wa nyuklia, alisema: “Hili ni chaguo ambalo Riyadh inapaswa kulichunguza kwa uzito na kwa umakini mkubwa.”

Pia aliongeza kuwa kupungua kwa nguvu na ushawishi wa Hezbollah nchini Lebanon baada ya vita na Israel, pamoja na kuanguka kwa utawala wa Bashar al-Assad nchini Syria mwaka jana, kumeipunguzia Iran uwezo wake wa kuathiri kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kisiasa na kiusalama katika eneo la Mashariki ya Kati.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha