8 Desemba 2025 - 14:14
Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Aendelea Kuitangaza Tanzania Katika Ajenda ya Elimu Duniani Kupitia Global Partnership for Education

Ushiriki wa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete katika majukwaa haya ya kimataifa unaonesha kwa vitendo dhamira yake endelevu ya kuitetea elimu kama nguzo kuu ya maendeleo ya binadamu, sambamba na kuendeleza diplomasia ya elimu kwa manufaa ya mataifa duniani, hususan Afrika.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) – ABNA: Brussels - Ubelgiji - Doha - Qatar | Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kimataifa ya Masuala ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education – GPE), ameendelea kuimarisha juhudi za maendeleo ya elimu duniani kupitia ushiriki wake katika mikutano muhimu ya kimataifa iliyofanyika nchini Ubelgiji na Qatar.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Aendelea Kuitangaza Ajenda ya Elimu Duniani Kupitia Global Partnership for Education

Katika mkutano wa GPE uliofanyika wiki hii mjini Brussels, Dkt. Kikwete alifanya mazungumzo maalum na Makamu Mwenyekiti wa GPE, Bi. Christine Hogan, yakilenga kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kuboresha elimu, hasa kwa nchi zinazoendelea. Aidha, alizungumza pia na Wajumbe wa Bodi ya GPE mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo, ambapo walijadili mwelekeo wa taasisi hiyo katika miaka ijayo. Katika kikao hicho, aliambatana na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE, Bi. Laura Frigenti.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Aendelea Kuitangaza Ajenda ya Elimu Duniani Kupitia Global Partnership for Education

Katika mwendelezo wa shughuli zake, Dkt. Kikwete pia alishiriki Mkutano wa 23 wa Kimataifa wa Doha nchini Qatar, ambapo alihudhuria mjadala wa ngazi ya juu pamoja na viongozi wakuu wa kimataifa akiwemo Rais Mstaafu wa Ghana, John Dramani Mahama, Khalifa Jassim Al Kuwari, Mkurugenzi Mkuu wa Qatar Fund for Development, pamoja na Achim Steiner, Msimamizi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Mjadala huo ulijikita katika nafasi ya elimu kama chachu ya maendeleo endelevu na ustawi wa jamii duniani.

Aidha, Dkt. Kikwete alifanya mazungumzo ya kibinafsi na Dkt. Hamad bin Abdulaziz Al Kawari, Waziri wa Nchi na Naibu Waziri Mkuu wa Qatar, wakati wa ziara hiyo mjini Doha. Mazungumzo yao yalilenga kuimarisha ushirikiano katika sekta ya elimu, maendeleo na ustawi wa jamii. Katika mazungumzo hayo, aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Balozi Habib Awesi Mohamed.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Aendelea Kuitangaza Ajenda ya Elimu Duniani Kupitia Global Partnership for Education

Ushiriki wa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete katika majukwaa haya ya kimataifa unaonesha kwa vitendo dhamira yake endelevu ya kuitetea elimu kama nguzo kuu ya maendeleo ya binadamu, sambamba na kuendeleza diplomasia ya elimu kwa manufaa ya mataifa duniani, hususan Afrika.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Aendelea Kuitangaza Ajenda ya Elimu Duniani Kupitia Global Partnership for Education

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha