Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Ikiwa uwezo wa mtu aliyewajibika kufunga ni wa kiwango ambacho kwa sababu ya udhaifu wa mwili au urefu wa siku, kufunga - hata kwa kupunguza shughuli na kuzingatia lishe - kunasababisha ugumu mkubwa usiovumilika, basi kwa tahadhari ya wajibu (iḥtiyāṭ wājib) anatakiwa kuweka nia ya kufunga; lakini akifikia hali ya mashaka au taabu kali sana, anaweza kufungua (kula/kunywa) na baadaye atalipa (qaḍā’) ya siku hiyo.
Pia, ikiwa ugumu huo mkubwa unatokana na shughuli kama kazi, masomo au kujisomea, kwa mujibu wa fatwa anatakiwa kufunga; na akifikia mashaka makubwa sana, anaweza kufungua na atalipa siku hiyo baadaye.
Your Comment