9 Juni 2026 - 21:45
Ghalibaf Atoa Ujumbe Maalumu Katika Maadhimisho ya Siku 100 za Jihadi ya Taifa la Iran

Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, amelipongeza taifa la Iran kwa msimamo wake wa kujitolea na kujitolea kulinda nchi, akisema umoja wa wananchi uliwavunja moyo maadui na kuiwezesha Iran kushinda changamoto kubwa.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- , Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mohammad Bagher Ghalibaf, ametoa ujumbe maalumu kwa munasaba wa kutimia siku 100 tangu kuanza kwa kile alichokiita “jihadi ya taifa la Iran” kwa ajili ya kulinda nchi na maslahi yake.

Katika ujumbe aliouchapisha kupitia ukurasa wake binafsi, Ghalibaf aliandika kuwa zimepita siku 100 tangu taifa la Iran lisimame kwa mshikamano na kujitolea kwa ajili ya kuilinda Iran.

Alisema: “Siku mia moja zimepita tangu jihadi ya taifa ambalo lilisimama kwa ajili ya kuilinda Iran mpendwa.”
Ghalibaf aliwashukuru wananchi wa Iran kwa mshikamano wao, akisema kuwa waliimarisha nguvu ya taifa, waliwavunja moyo maadui na kuzuia mipango iliyolenga kuilazimisha Iran kusalimu amri.

Aidha, alieleza kuwa umoja na uthabiti wa wananchi uliiwezesha Iran kujinasua kutoka katika vitisho vya maadui ambao walikuwa wamejipanga kuishinikiza na kuidhoofisha Jamhuri ya Kiislamu.

Mwisho wa ujumbe wake, Spika huyo wa Bunge alitoa salamu za kuipongeza Iran na wananchi wake kwa kusema: “Mwenyezi Mungu awabariki nyinyi mlioipa Iran nguvu, mkawakatisha tamaa maadui na kuinusuru nchi kutoka kwenye makucha ya maadui waliokuwa wamejipanga kuiangamiza. Daima idumu Iran, na iishi milele harakati ya mapambano ya taifa kubwa la Iran.”

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha