18 Juni 2026 - 18:10
Sheikh Naim Qassem: Iran ni Alama ya Heshima na Nguzo ya Muqawama Dhidi ya Israel

Katibu Mkuu wa Hezbollah, Sheikh Naim Qassem, amesema katika barua yake kwa Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Qalibaf, kwamba Iran imeonyesha kwa vitendo uungaji mkono wake kwa haki, muqawama na waliodhulumiwa. Ameeleza kuwa mchango wa Iran umeimarisha uwezo wa Lebanon kujitetea na kuitaja Iran kuwa "alama ya heshima na utukufu" katika kukabiliana na utawala wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) -ABNA-, Katibu Mkuu wa Hezbollah nchini Lebanon, Sheikh Naim Qassem, ametuma barua kwa Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Bagher Qalibaf, akielezea shukrani na kupongeza nafasi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuunga mkono harakati za mapambano dhidi ya uvamizi wa Israel.

Katika barua hiyo, Sheikh Naim Qassem amesema kuwa Iran imegeuza matumaini ya pekee ya kuzuia uchokozi wa Marekani na Israel dhidi ya Lebanon kuwa uhalisia, na kuidhihirishia dunia kwamba inasimama upande wa haki, muqawama (mapambano ya upinzani) na watu wanaodhulumiwa. Aliongeza kuwa iwapo mataifa mengine yangefuata msimamo huo, Marekani na Israel visingekuwa na ujasiri wa kuendeleza uchokozi wao, wala uvamizi wa Kizayuni usingedumu katika ardhi za Palestina na Al-Quds.

Aidha, Sheikh Qassem alisisitiza kuwa Iran imeipatia Lebanon uwezo na nyenzo za kukomboa ardhi yake, kuponya majeraha ya jamii na kuwasaidia wananchi wake. Alisema kuwa leo Iran inatoa damu ya watoto wake na inakabiliana moja kwa moja na utawala wa Kizayuni kutokana na mashambulizi yake dhidi ya eneo la Dahieh, kusini mwa Beirut, huku ikibeba gharama kubwa za vita.

Akihitimisha ujumbe wake, Katibu Mkuu wa Hezbollah alisema kwa msisitizo: "Iran ni alama ya heshima, utukufu na hadhi."

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha