3 Julai 2026 - 11:43
Ujumbe wa Wanazuoni wa Palestina Wawasili Iran Kutoa Heshima kwa Mwili Msafi wa Shahidi aliyeishi kwa kutetea Quds na Watu wa Palestina

Ujumbe wa masheikh na wanazuoni kutoka Palestina umewasili Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ajili ya kutoa heshima na kuonesha mshikamano wao kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kiongozi Mkuu wa Iran Shahidi Sayyid Ali Khamenei (ra); huku ukisisitiza nafasi ya Kiongozi huyo wa Mapinduzi ya Kiislamu katika kuunga mkono Quds Tukufu na haki za wananchi wa Palestina.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– ujumbe wa masheikh na wanazuoni kutoka Palestine umefika katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ajili ya kutoa heshima na kuimarisha mshikamano wa Kiislamu katika mazingira ya majonzi na mapambano ya Umma.
 
Ujumbe wa Wanazuoni wa Palestina Wawasili Iran Kutoa Heshima kwa Mwili Msafi wa Shahidi aliyeishi kwa kutetea Quds na Watu wa Palestina

Ujumbe huo umesisitiza nafasi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Husayni Khamenei, katika kuunga mkono wananchi wa Palestina na kusimama imara katika ulinzi wa Jerusalem na maeneo matakatifu ya Kiislamu.
 
Aidha, wanazuoni hao wameeleza umuhimu wa kuimarisha umoja wa Waislamu duniani na kuendeleza msimamo wa pamoja katika kupinga uonevu, huku wakisisitiza kuendelea kwa mshikamano kati ya wanazuoni na harakati za ukombozi wa Palestina.
 
Hafla hiyo imeelezwa kuwa ni ishara ya uhusiano wa kiroho na kisiasa kati ya pande mbalimbali za Umma wa Kiislamu katika kuunga mkono haki na uadilifu duniani.

Ujumbe wa Wanazuoni wa Palestina Wawasili Iran Kutoa Heshima kwa Mwili Msafi wa Shahidi aliyeishi kwa kutetea Quds na Watu wa Palestina

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha