4 Julai 2026 - 21:52
Picha ya Kihistoria ya Mwili Mtukufu wa Kiongozi Shahidi Imam Sayyid Ali Khamenei Yashuhudiwa Jijini Tehran

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) – ABNA – limechapisha picha ya karibu zaidi ya mwili mtukufu wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Shahidi Ayatullah Mkuu Imam Sayyid Ali Khamenei (Qudsallahu Nafsahu Az-Zakiyyah), katika ukumbi wa Msikiti wa Imam Khomeini (Quds Sirruh), huku mamilioni ya watu duniani wakiendelea kuomboleza na kumuenzi kama “Imamu wa Wanyonge”.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) – ABNA – Picha ya kihistoria na ya karibu zaidi ya mwili mtukufu wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Shahidi Ayatullah Mkuu Imam Sayyid Ali Khamenei (Qudsallahu Nafsahu Az-Zakiyyah), imechapishwa leo Jumamosi, tarehe 4 Julai 2026, katika ukumbi wa Msikiti wa Imam Khomeini (Quds Sirruh) mjini Tehran.

Picha hiyo imeibua hisia kubwa za huzuni na majonzi miongoni mwa mamilioni ya wapenzi wa Ahlul-Bayt (as), Waislamu na watu huru duniani, ambao wameendelea kumkumbuka kiongozi huyo shahidi kwa mchango wake mkubwa katika kutetea Uislamu, kuunga mkono harakati za mapambano dhidi ya dhulma na kusimama pamoja na wanyonge wa dunia.

Watu wengi wameitaja picha hiyo kuwa ni “taswira ya milele” inayobeba kumbukumbu za kiongozi aliyekuwa nembo ya ujasiri, msimamo na mapambano dhidi ya ubeberu na Uzayuni.

Katika ujumbe unaoambatana na picha hiyo, waumini wamehimizwa kusimama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kushiriki katika shughuli za kumuaga na kumzika “Imamu wa Wanyonge”, huku kaulimbiu ya #QumuuLillah (Simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu) na #Tashii_Imam_Al-Mustadhafin (Mazishi ya Imamu wa Wanyonge) ikiendelea kusambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha