Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) – ABNA – Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu, Hujjatul-Islam Hamid Shahriari, amesisitiza kuwa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Imam Sayyid Ali Khamenei, aliuona umoja wa Umma wa Kiislamu kuwa ni mkakati wa msingi wa kukabiliana na utawala wa mabavu, uistikbari wa kimataifa na njama za maadui za kueneza mifarakano.
Akizungumza na Shirika la Habari la IRNA pembezoni mwa hafla ya kuuaga mwili wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Sheikh Shahriari alisema kuwa sherehe kubwa za kuuaga na kuusindikiza mwili wa kiongozi huyo zimeunda tukio la kihistoria la kuhuisha upya ahadi ya wananchi wa Iran kwa misingi ya Uislamu halisi, Wilayah, uhuru na muqawama.
Ameeleza kuwa mahudhurio makubwa na yasiyokuwa ya kawaida ya wananchi kutoka matabaka na mitazamo mbalimbali yameonyesha tena kwamba imani, umoja na uaminifu kwa tunu za Mwenyezi Mungu ndiyo mtaji mkubwa wa taifa la Iran, na kwamba mtaji huo utaendelea kuwa imara na usiovunjika hata katika nyakati ngumu na mitihani mikubwa zaidi.
Your Comment