9 Julai 2026 - 19:24
Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi: Wageni Hawana Haki katika Mlango wa Hormuz

Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC Navy) limesema kuwa mataifa ya kigeni hayana haki yoyote katika eneo la Iran na Mlango wa Hormuz, likionya kuwa hatua za kijeshi za Marekani zinatishia usalama wa njia hiyo muhimu ya kimataifa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Jeshi la Wanamaji la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC Navy) limetangaza kuwa mataifa ya kigeni hayana nafasi wala haki yoyote katika ardhi ya Iran na Mlango wa Hormuz, likisisitiza kuwa usalama wa eneo hilo utalindwa na vikosi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika taarifa iliyotolewa Alhamisi, jeshi hilo limesema kuwa kile lilichokiita vitendo vya uchokozi na uingiliaji wa jeshi la Marekani katika kuelekeza njia za meli zinazopita katika Mlango wa Hormuz vinavuruga mchakato wa kufunguliwa kwa njia hiyo hatua kwa hatua na vinaweka katika hatari maslahi ya nchi zinazotegemea njia hiyo muhimu ya baharini.

Jeshi hilo pia liliipongeza wananchi wa Iran kwa ushiriki wao mkubwa katika mazishi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeuawa shahidi nchini Iran na Iraq, likisema kuwa umati huo wa mamilioni umeonesha kuwa enzi ya kiburi cha madola makubwa inaelekea ukingoni, na kwamba karne ya sasa ni ya ushindi wa matakwa na irada ya mataifa.

Aidha, taarifa hiyo ilisisitiza kuwa vikosi vya Iran vitaendelea kulinda usalama wa maji ya eneo hilo na maslahi ya taifa, huku vikitoa onyo dhidi ya hatua zozote za kigeni zitakazoongeza mvutano katika Ghuba ya Uajemi na Mlango wa Hormuz.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha