-
Inna Lillah wa Inna Ilayhi Rajiun:
Na Mwisho Mwema ni wa Wale Wamchao Mwenyezi Mungu
Marhuma, Ukthti Fatima Mwiru, Miaka yote mpaka mwisho wa Uhai wake, alikuwa mstari wa mbele katika utumishi bora uliotuka wa kuhudumia Uislamu na Waislamu, na alikuwa ni Kinara Mtetezi wa Haki za Wanyonge na Wadhulumiwa wa Palestina, kwa kupaza Sauti yake katika Jamii ya Wanawake na Watu wote katika kuungana na Wanawake na Watoto wa Palestina wanaokumbana na Mauaji ya Kimbari ya Utawala Haram wa Kizayuni.
-
Rais Putin: Watu wa Magharibi hawaielewi Russia
Rais Vladimir Putin amesema baadhi ya watu katika nchi za Magharibi hawaielewi Russia, lakini amesisitiza kuwa ukweli huo hauwezi kutatiza hata kidogo ustawi na maendeleo ya nchi hiyo.
-
Marekani na Ulaya zashindwa kukabiliana na changamoto za kimataifa
Mark Rutte, Katibu Mkuu wa NATO amesisitiza juu ya umoja wa pande mbili za Bahari ya Atlantiki na kusema kuwa changamoto za kiusalama duniani ni kubwa kiasi kwamba Ulaya na Marekani pake yazo haziwezi kukabiliana nazo.
-
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Glasgow wagoma kula katika kuihami Gaza
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha serikali cha Glasgow, Scotland wamefanya mgomo wa kula wakilalamikia ushirikiano wa chuo hicho na makampuni yanayotengeneza silaha kwa ajilii ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Yemen yautwanga kwa makombora utawala wa Kizayuni/sauti za ving'ora zasikika
Duru za Kizayuni zimearifu kuwa sauti za ving'ora vya hatari vilisikika jana katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) kufuatia shambulio la makombora ililotekelewa na jeshi la Yemen.
-
Radiamali ya Hamas kufuatia kuuliwa shahidi "Abdel-Latif al-Qanoua" katika hujuma ya Israel
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imeashiria katika taarifa yake kuhusu kuuawa shahidi Abdel-Latif al-Qanoua Msemaji wa harakati hiyo katika shambulio la utawala wa Kizayuni na kutangaza kuwa: "Kuwalenga kwa masambulizi viongozi wa harakati ya Hamas na wasemaji wake kamwe hakuwezi kuvunja irada yetu.
-
Kilele cha ukatili wa Israel; Waliouawa shahidi Gaza wapindukia 50,200
Jeshi katili la Israel ambalo lilianzisha mashambulizi mapya ya anga katika Ukanda wa Gaza mnamo Machi 18, limeendelea kupuuza miito ya jamii ya kimataifa ya kukomesha ukatili wake katika ukanda huo; ambapo mpaka sasa limeshaua shahidi Wapalestina karibu 900 na kujeruhi wengine karibu 2,000.
-
Al Houthi: Mashambulizi ya Marekani hayawezi kubadilisha msimamo wa Yemen
Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza kuwa nchi hiyo ya Kiarabu itaendelea na misimamo yake isioyumba wa kuwahami Wapalestina na mapambano yao halali ya ukombozi bila kujali ukubwa wa mashambulizi ya kijeshi wa Marekani.
-
Zainab Nasrullah: Kuwauwa viongozi wa Muqawama hakutadhoofisha mapambano
Binti wa Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, aliyekuwa Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa kuwauwa viongozi wa Muqawama hakutadhoofisha mapambano ya ukombozi.
-
Marajii Taqlidi na Maulamaa watoa wito wa kushiriki katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds
Marajii Taqlidi na Maulamaa nchini Iran wamesisitiza juu ya kushiriki pakubwa na kwa hamasa wananchi katika maandamano ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya quds.
-
Kiongozi Muadhamu: Siku ya Quds ya mwaka huu itakuwa ya aina yake
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu yanayofanyika leo Ijumaa ya Machi 28 kote duniani yana umuhimu mkubwa kuliko miaka iliyopita.
-
Mamilioni ya Wairani washiriki maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds
Wananchi Waislamu wa Iran kote nchini wamejitokeza kwa mamilioni kushiriki katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds, kuonyesha mshikamano na Palestina, na kulaani ukatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina hasa katika Ukanda wa Gaza.
-
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds
Mnamo mwaka 1979, mara tu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini alitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa siku ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds, akiwa amesimama imara katika kupigania haki za watu wote wanaodhulumiwa ulimwenguni.
-
Jibu la Iran kwa barua ya Trump/ Araqchi: Mazungumzo chini ya mashinikizo hayana maana
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Iran amesisitiza kwamba mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani kuhusu mpango wa amani wa nyuklia wa nchi hiyo hayana maana maadamu sera ya "shinikizo la juu" na vitisho vya kijeshi bado vipo.
-
Cuba: Uhamiaji umekuwa biashara kwa Marekani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba amepinga viza ya kadi ya dhahabu ya kupewa makazi mkabawa wa dola milioni tano ya Marekani, na kuituhumu serikali ya Trump kwa kutumia suala la uhamiaji kama biashara, kwa kuuza nyumba na kuwafukuza wahamiaji haramu.
-
Imam wa Swala ya Ijumaa: Maandamano ya Siku ya Quds ni dhihirisho la Tauhidi na kumpenda Mungu
Imam wa Swala ya Ijumaa ya leo katika mji wa Tehran ameashiria kushiriki kwa wingi na kwa hamas wananchi wa Iran ya Kiislamu katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu na kusema: Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds siku zote yamekuwa dhihirisho la Tauhidi na kumpenda Mwenyezi Mungu.
-
Ni ipi kati ya ibara hizi mbili iliyo sahihi? "Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Itrah wangu, Ahlul-Bayt wangu au Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna yangu"
Hadithi sahihi na iliyothibitishwa kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni yenye lafdhi hii isemayo: «وأهل بیتي» / "Na Ahlul-Bayt wangu”, ama riwaya ile ambayo imepachikwa lafdhi au neno «وسنّتي» / “Na Sunna yangu” badala ya lafdhi ya asili na sahihi isemayo: «وأهل بیتي» / "Na Ahlul-Bayt wangu”, riwaya hiyo ni batili kwa mtazamo wa sanadi ya upokezi wa Hadithi husika.
-
Kiongozi wa Mapinduzi: Maandamano ya Mwaka huu yatakuwa miongoni mwa Maandamano yenye Heshima Kubwa katika Siku ya Quds
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Mwenyezi Mungu akipenda (Insha Allah), Matembezi (Maandamano) ya Mwaka huu yatakuwa miongoni mwa Matembezi bora zaidi, Matukufu na yenye Heshima Kubwa katika Siku ya Quds.
-
Mwaliko (Wito) wa Ayatollah Ramadhani kwa watu wa Gilan Kushiriki Katika Maandamano ya Siku ya Quds ya 2025
Ayatollah "Reza Ramezani", Mwakilishi wa Wananchi wa Gilan katika Baraza la Wataalamu wa Uongozi, katika Mkesha wa Siku ya Quds Duniani, amewaalika na kuwahimiza watu kushiriki katika Maandamano ya Siku hii.