-
Maandamano yarindima Meya wa Istanbul, hasimu wa Rais wa Uturuki alipokamatwa
Maelfu ya wananchi wa Uturuki wamemiminika barabarani kulalamikiwa kutiwa mbaroni Meya wa Istanbul, Ekrem Imamoglu, mpinzani mkuu wa kisiasa wa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ambaye amekamatwa kwa tuhuma za rushwa na ugaidi; siku chache kabla ya kuteuliwa kuwa mgombea wa urais.
-
Netanyahu: Mashambulio yalioua watoto 174 Gaza ni mwanzo tu
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ametangaza kushadidi mashambulio mabaya dhidi ya Gaza, akionya kwamba mashambulizi ya hivi karibuni ya anga, ambayo yaliua watoto wasiopungua 174 katika ukanda huo, ni mwanzo tu wa uchokozi mkubwa zaidi dhidi ya Wapalestina.
-
Saudia: Israel inahatarisha usalama na utulivu wa eneo zima
Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudia imesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel unatishia usalama na utulivu wa eneo hili zima na kwamba jamii ya kimataifa na Baraza la Usalama zina wajibu wa kutekeleza majukumu yao ipaswavyo na kusimama kidete kukabiliana na hujuma za Israel huko Palestina na Syria.
-
San'a: Iran haiingilii hata chembe maamuzi ya Yemen
Waziri wa Mambo ya Nje wa Yemen amesisitiza kuwa: Iran haingilii hata chembe maamuzi ya serikali ya San’a na kwamba operesheni za Yemen dhidi ya Wazayuni ni uamuzi huru na utaendelea kutekelezwa kivitendo hadi mzingiro wa Ghaza utakapovunjwa kikamilifu.
-
Israel yaua watu wengine 71 katika mashambulizi dhidi ya Gaza na kuikalia tena Netzarim
Ripoti zinaonyesha kuwa ndani ya saa 24 zilizopita wanajeshi wa Israel wamewaua shahidi Wapalestina zaidi ya 71 katika miji ya Beit Lahiya, Rafah na Khan Yunis, huku wengine wengi wakijeruhiwa.
-
Makundi ya muqawama yasisitiza kuunganisha juhudi ili kukabiliana na mashambulizi ya Israel
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) na Harakati ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina (PFLP) zimesisitiza juu ya haja ya kuunganisha juhudi makundi ya muqawama ya Palestina na nchi za Kiarabu ili kukabiliana na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na kuunga mkono mapambano ya ukombozi katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza na kupinga mipango ya Marekani na utawala wa Kizayuni ya kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina.
-
Kiongozi wa Mapinduzi: Mwaka 1404 ni "Mwaka wa Uwekezaji kwa ajili ya Uzalishaji"
Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu uwa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe kwa mnasaba wa kuanza mwaka mpya wa 1404 hijria shamsia na kuutaja mwaka huu mpya kuwa ni "Mwaka wa Uwekezaji kwa ajili ya Uzalishaji."
-
'Waislamu wachukue msimamo wa maana dhidi ya mauaji ya kimbari yanayofanywa na Wazayuni'
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Iraq ya An-Nujabaa imelaani mashambulizi ya kinyama yaliyoanzishwa tena na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza na kuwataka Waarabu na Waislamu duniani kote wachukue misimamo thabiti dhidi ya hujuma hizo.
-
Maafisa 5 waandamizi wa HAMAS wauawa shahidi katika mashambulio ya Israel Ghaza
Maafisa watano waandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS wameuawa shahidi kufuatia mashambulizi ya kinyama yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza.
-
Hamas: Marekani ni mshirika wa moja kwa moja katika vita dhidi ya watu wa Gaza
Msemaji wa harakati ya Hamas amesema harakati hiyo inatekeleza kikamilifu masharti ya makubaliano ya usitishaji vita na kwamba Wazayuni wameyakiuka akisisitiza kuwa, uratibu wa awali wa utawala huo ghasibu na Washington wa kuanzisha tena vita dhidi ya watu wa Gaza unaashiria ushiriki wa moja kwa moja wa Marekani katika jinai zinazofanywa Wazayuni.
-
Al Houthi: Israel inapanga kushambulia nchi zingine ikiwa itaangamiza Palestina
Kiongozi wa harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen ameonya kuwa utawala ghasibu wa Israel utaanza kushambulia nchi nyingine ikiwa utafanikiwa kuangamiza juhudi za ukombozi za Palestina dhidi ya ukaliaji na uchokozi wake, huku akipendekeza hatua za kijeshi na nchi za Kiarabu na Kiislamu dhidi ya utawala huo.
-
Dunia yakasirishwa na hatua ya Israel kuendeleza vita dhidi ya Gaza
Jamii ya kimataifa imebainisha hasira yake baada ya utawala katili wa Israel kuendelea na mashambulizi ya anga dhidi ya Gaza, huku ikivunja makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyokuwa na lengo la kumaliza mzozo wake wa miezi 17 na Hamas.
-
Rais wa China akataa mwaliko wa EU wa kuhudhuria kikao cha kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano
Rais Xi Jinping wa China amekataa mwaliko wa kuhudhuria kikao kilichopangwa kufanyika mjini Brussels kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi yake na Umoja wa Ulaya.
-
Vikosi vya Ulinzi vya Yemen vyaishambulia kwa mara ya pili manowari ya kubebea ndege za kivita ya US
Vikosi vya Ulinzi vya Yemen vimeishambulia kwa mara ya pili manowari ya kubebea ndege za kivita ya Marekani ya USS Harry Truman na kuzima mashambulizi ya anga yaliyokuwa yamedhamiriwa kufanywa na Washington dhidi ya nchi hiyo.
-
Hamas: Vitisho vya Marekani vinatatiza zaidi hali ya mambo
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesisitiza kuwa: Vitisho vya Marekani vinapelekea tu hali ya mambo kuwa ngumu zaidi.
-
Mauaji ya raia 2 wa Lebanon kupitia magaidi wa Al-Julani
Magaidi wa Al-Julani wamefanya jinai nyingine katika maeneo ya mpakani mwa Lebanon na Syria.
-
Video | Uwekaji wa Meza ya Iftar katika Mji wa mpakani Kusini mwa Lebanon
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (A.S) - Abna – Meza ya chakula cha Iftar kwa wafungaji wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, iliwekwa katika Uwanja Mkuu wa mpaka wa Mji wa "Al-Khayyam" Kusini mwa Lebanon. Wakati wa vita vya hivi karibuni, Mji huu ulikuwa mlengwa wa mashambulizi makali zaidi ya anga na ardhini ya jeshi haram la Kizayuni.
-
Katika kukabiliana na mashambulizi ya Marekani... Yemen inakabiliana na ongezeko la mvutano kwa ongezeko la mvutano
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA -: Vikosi vya jeshi la Yemen vimelenga (vimeishambulia) Meli ya kubebea ndege za Kivita ya USS Truman katika Bahari Nyekundu kwa mara ya pili ndani ya masaa 24 kwa kutumia Makombora ya Balistiki na Mbawa na Droni (Ndege za mashambulkizi zisizokuwa na rubani). Kiongozi wa vuguvugu la Ansarullah la Yemen, Sayyid Abdul Malik Al-Houthi, amethibitisha kuwa Yemen itakabiliana na hali yoyote ya ongezeko la kasi ya mvutano kwa ongezeko la kasi ya mvutano.
-
Radiamali ya Seneta RajA Nasser kwa mauaji ya Mwanazuoni wa Pakistan
Mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan amelaani mauaji ya Mufti Munir Shakir, Mwanazuoni wa Kisunni wa Pakistan, na kuyataja kuwa ni hasara isiyoweza kufidiwa.
-
Sayyid Abdul Malik al-Houthi: Meli za Marekani ni marufuku pia kupita Bahari Nyekundu
Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema: Tutajibu ongezeko la mvutano kwa ongezeko la mvutano. Kuanzia sasa, sambamba na kupiga marufuku kupita kwa meli za Israeli katika Bahari Nyekundu, kupita kwa meli za Marekani pia ni marufuku.
-
Habari Pichani | Sherehe ya kuzaliwa kwa Imam Hassan al-Mujtaba (a.s) katika Haram Tukufu la Imam Ali (a.s)
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - Abna -, Kwa mnasaba wa kuzaliwa kwa Imam Hassan al-Mujtaba (a.s), sherehe ya hadhara kubwa ya watu imefanyika katika Madhabahu (Haram) Tukufu ya Imam Ali (a.s) kwa kuhudhuriwa na Mazuwwari na kundi la Wasomi, Wataalamu wa Mashairi, Maveterani na Mahudumu wa Shaairi za Husseini (as).
-
Ripoti ya Picha | Iftar kwenye Magofu ya Msikiti wa Salim Abu Muslim huko Beit Lahia
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) - Abna -, Wapalestina wanaoishi Beit Lahia Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza wanafturu katika mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwenye Magofu ya Msikiti wa Salim Abu Muslim. Ikumbukwe kuwa Msikiti wa Salim Abu Muslim huko Beit Lahia uliharibiwa katika mashambulizi ya majeshi haram ya Kizayuni.
-
Video | Upangaji wa maua kwenye Haram Tukufu ya Imam Ali (a.s) katika Masiku ya Kuzaliwa kwa Imam Hassan al-Mujtaba (a.s)
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna- Haram Tukufu ya Amir al-Muuminin Ali (a.s) imepambwa kwa maua mazuri katika mnasaba wa Siku ya Kuzaliwa kwa Imam Hassan al-Mujtaba (a.s).
-
Onyo la Baraza la Wawakilishi la Yemen: Vikosi vya jeshi vitajibu ipasavyo
Baraza la Wawakilishi la Yemen limetoa taarifa likionya kuhusu matokeo ya hujuma za Marekani na Uingereza dhidi ya raia wa nchi hii.
-
Mustakbali uliogubikwa na kiza wa Syria; wafuasi wa al Julani wazidi kuua raia
Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Syria limeripoti habari ya kuuawa zaidi ya raia 1,383 wasio na hatia katika shambulio lililofanywa na magenge yenye mfungamano na watawala wa hivi sasa wa Syria kwenye maeneo ya Waislamu wa Kishia, magharibi mwa nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Associated: Marekani na Israel zilitaka kuwapa makazi wakazi wa Gaza katika nchi tatu za Kiafrika
Shirika la habari la Associated Press limeripoti kuwa Marekani na Israel zilitoa pendekezo kwa maafisa wa nchi tatu za Afrika la kuwapa makazi Wapalestina kutoka Ukanda wa Gaza kwenye ardhi za nchi hizo.
-
Waumini 80,000 wa Kipalestina washiriki Swala za Ijumaa katika Msikiti wa Al-Aqsa
Waumini wapatao 80,000 wa Kipalestina walishiriki swala ya Ijumaa ya pili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani katika Msikiti wa Al-Aqsa jijini Al Quds (Jerusalem) licha ya vizuizi vikali vilivyowekwa na Israel kuwazuia Waislamu kufika katika eneo hilo takatifu.
-
Hamas yalaani marufuku ya pamoja ya US na EU dhidi ya al Aqsa TV
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani uamuzi uliochukuliwa na Marekani na Umoja wa Ulaya wa kupiga marufuku matangazo ya televisheni ya al Aqsa.
-
Uwepo wa magaidi kutoka nchi 20 katika Serikali ya Syria | Serikali ya mpito au Mradi wa Kikoloni!
Vyanzo vyenye maarifa na utambuzi, vimetoa taarifa juu ya kuundwa kwa muundo mpya wa usalama katika utawala wa Kigaidi wa al-Jolani.
-
Habari Pichani | Hamas: Kusimamisha idhaa ya al-Aqsa ni jaribio la kudhibiti sauti ya Wapalestina
Mtandao wa satelaiti wa Al-Aqsa umetangaza: Matangazo ya Idhaa ya Al-Aqsa yamesimamishwa katika Satelaiti zote za Kimataifa. Na Shirika lolote la Satelaiti litakaloendelea na urushaji wa matangazo na habari za Idhaa ya Al-Aqsa litakumbana na vikwazo vikubwa vya kiuchumi.