Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Siku ya Alhamisi, Utawala wa Kizayuni (Israel) ulidai kuwa umevamia makao ya makamanda wa Kiyemeni mjini Sana’a na kuwaua makamanda na viongozi wengi wa Yemen.
Hata hivyo, madai haya yamekanushwa na uongozi wa juu wa harakati ya Ansarullah pamoja na maafisa wengine wa Yemeni, ambao wamesisitiza kuwa mashambulizi ya kinyama ya Israel yamelenga tu maeneo ya kiraia.
Katika muktadha huu, viongozi wawili wa Kiyemeni - Abdulaziz al-Bakr, waziri wa zamani mshauri wa serikali ya Sana’a na Katibu Mkuu wa chama cha “Ujamaa wa Kitaifa” (Socialist Nationalist Party), pamoja na Hizam al-Asad, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Ansarullah - walizungumza na shirika la habari la Abna na wakikanusha madai ya Israel huku wakisisitiza juu ya kuendelea kwa mapambano ya Wayemeni.
Walisema: “Kila shambulio linalowalenga raia huko Sana’a linaongeza nguvu na ari ya wananchi wa Yemen katika harakati ya mapambano.”
Al-Bakr alisema:
Madai yaliyotolewa na adui Mzayuni ni ya uongo kabisa na hayana uhusiano wowote na kulenga viongozi wa kijeshi au maeneo ya kijeshi nchini Yemen. Uhalisia wa kijeshi unathibitisha kuwa mashambulizi yote ya hivi karibuni yalilenga tu miundombinu ya kiraia na huduma kama vile vituo vya umeme, kampuni za mafuta, au maeneo yasiyo na watu ambayo tayari yalikuwa yameshambuliwa hapo awali.
Hali hii inaonyesha kuwa adui ameshindwa kijasusi na hana uwezo wa kupata taarifa sahihi kuhusu maeneo ya kijeshi au uongozi wa Yemen. Lengo lake kuu ni kuwalenga raia wa Yemen na uwezo wao wa kiraia, kwa jaribio la kuwalazimisha kunyenyekea na kuwaadhibu kwa sababu ya msimamo wao wa kuunga mkono Palestina na Gaza.
Al-Bakr aliongeza: Dakika chache baada ya uvamizi huo, Wizara ya Ulinzi ya Yemen ilikanusha taarifa za uongo kuhusu kulengwa kwa viongozi wa Sana’a na kuthibitisha kuwa madai hayo ni batili.
Akasema zaidi kuwa Israel inalenga kufikia malengo kadhaa kwa kupitia madai haya:
-
Kutengeneza ushindi wa uongo ili kuficha kushindwa kwake kwenye uwanja wa vita dhidi ya muqawama wa Palestina;
-
Kujaribu kuathiri hali ya kisaikolojia ya wananchi wa Yemen, kwa kudai kuwa wana uwezo wa kuwalenga viongozi wao – hali ambayo si ya kweli;
-
Kutumia madai haya kwa propaganda ya ndani ya kisiasa na kuwahadaa washirika wake wa Kimarekani na Magharibi, kwa lengo la kuhalalisha uvamizi wake unaoendelea na kushindwa kwake kwa mara kwa mara.
Kwa maneno mengine, kile ambacho adui anafanya ni udanganyifu na kupindisha ukweli ili kuficha udhaifu wake wa kijeshi.
Katibu Mkuu wa chama cha Ujamaa wa Kitaifa wa Yemen aliendelea kusisitiza kuwa:
Msimamo wa Ansarullah na majeshi ya Yemen ni wazi na thabiti — mashambulizi haya hayawezi kuizuia Yemen kuendelea na operesheni zake za kijeshi kwa ajili ya kuisaidia Gaza hadi pale uvamizi utakapokoma na mzingiro kuondolewa.
Majeshi ya Yemen yameeleza mara kadhaa kuwa yatajibu mashambulizi haya kwa wakati na mahali mwafaka, na kwamba orodha ya malengo yao baharini na nchi kavu ipo hai na tayari kutekelezwa.
Ansarullah kwa upande wake wamesisitiza kuwa jinai hizi za Israel zinaongeza tu dhamira ya Wayeyemeni kuendelea kuishikilia Palestina kama suala kuu la kitaifa na kuunga mkono mapambano kwa nguvu zote. Kifupi, adui ameshindwa kutimiza malengo yake, bali amechochea chaguo la mapambano zaidi ndani ya Yemen.
Al-Bakr alihitimisha kwa kusema:
“Wananchi wa Yemen, tangu mwanzo wa uvamizi, wamedhihirisha kuwa hawashindiki wala hawanyenyekei. Kadri mashambulizi ya Kizayuni na Kimarekani yanavyozidi, ndivyo mshikamano wa watu na uungwaji mkono wa muqawama unavyoimarika. Leo hii, Wayeyemeni wanaona mashambulizi haya kama uthibitisho wa nafasi yao kuu katika vita dhidi ya mradi wa Kizayuni-Kimarekani.”
Akasema kuwa majibu ya wananchi ni kama ifuatavyo: Maandamano ya hasira, kutoa msaada wa binadamu, fedha na silaha kwa uwanja wa vita, pamoja na kuinua ari ya wapiganaji wa muqawama.
Afisa huyo wa Yemen alisisitiza tena kuwa: “Kila shambulio linalowalenga raia Sana’a au mahali popote linakuwa kama mafuta zaidi kwenye moto wa mapambano ya Wayeyemeni hadi ushindi wa mwisho upatikane.”
Hizam al-Asad: “Kutengeneza ushindi wa kufikirika kunaonyesha kiwango cha kushindwa kwa Israel kijasusi, kijeshi na kimaadili.”
Katika majibu yake kuhusu madai ya Israel ya kushambulia makao ya makamanda wa Yemen, Hizam al-Asad alisema kuwa hakuna ukweli wowote katika madai hayo, na kwamba ni ushahidi wa kushindwa kwa Israel katika nyanja zote – kijasusi, kijeshi, na hata kimaadili — huku ikijaribu tu kuunda hadithi za ushindi wa bandia.
Alisisitiza kuwa uvamizi wa Israel umelenga tu maeneo ya kiraia, vituo vya huduma, au maeneo yaliyoshambuliwa mara kadhaa hapo awali, na kwamba juhudi zote za Israel za kuwazuia Wayeyemeni kuisaidia Gaza zimegonga mwamba.
Alisema: “Wananchi wa Yemen, kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu, wameamua kuendelea kuiunga mkono Gaza hadi uvamizi utakapoisha na mzingiro kuondolewa.”
Your Comment