Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Hassan Fadlallah, mwakilishi mwandamizi wa Hezbollah katika Bunge la Lebanon, amesema:
Rais wa Marekani anadhani kuwa anaongoza au anaidhibiti dunia, lakini pale anapokuwepo kiongozi jasiri, mwenye hekima na shujaa, na pale kunapokuwepo taifa lililo thabiti na lenye msimamo wa mapambano, mipango na njama zote huvunjika katika kizingiti cha taifa hilo.
Sisi tumeazimia kwamba uchaguzi wa Bunge la Lebanon utafanyika kwa wakati wake wa kisheria bila nyongeza wala kuahirishwa.
Jaribio lolote la nje la kuuchelewesha kwa lengo la kubadilisha mizania ya ndani au kudhoofisha ngome ya muqawama (harakati za upinzani) halitafanikiwa.
Your Comment