4 Juni 2026 - 17:54
Ghadir Khum: Kwa Nini Mtume (s.a.w.w.) Alikusanya Maelfu ya Waislamu Kumtangaza Imam Ali (a.s.)?

Kwa mujibu wa Madrasatu Ahlul-Bayt (a.s.), tukio la Ghadir Khum halikuwa la kutangaza mapenzi na heshima kwa Imam Ali (a.s.) pekee, bali lilikuwa tangazo la Mwenyezi Mungu kuhusu Wilayah na uongozi wake baada ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.), jambo linalodhihirisha umuhimu wa kuwepo kwa kiongozi wa Umma baada ya Mtume (saww).

Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Alhamdulillah ambaye ametujaalia kuwa miongoni mwa wenye kushikamana na Wilayah ya Amirul-Muuminina, Ali bin Abi Talib (a.s).

Hakika kuwepo kwa kiongozi wa Umma baada ya Mtume (s.a.w.w.) ni jambo linalokubaliwa na akili iliyosalama na linalohitajika kwa mujibu wa maumbile ya kawaida ya mwanadamu.

Na wa kwanza kuona umuhimu wa kuwepo kwa kiongozi wa Umma baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ni Mwenyezi Mungu (S.W.T.) Mwenyewe. Ndiyo maana akamuamrisha Mtume Wake (s.a.w.w.) atangaze Wilayah na uongozi wa Imam Ali bin Abi Talib (a.s.) katika tukio la Ghadir Khum.

Kwa msingi huo, tukio la Ghadir Khum halikuwa mkusanyiko wa kawaida wa kuwatangazia Waislamu wampende Imam Ali (a.s.) au wamheshimu, hadi maelfu ya watu wakusanywe katika sehemu na wakati huo maalumu. Bali ujumbe wake ulikuwa mkubwa zaidi na wa kina zaidi kuliko hilo.

Hasa tukizingatia kwamba mapenzi, fadhila na nafasi ya Imam Ali (a.s.) tayari vilikuwa vinajulikana miongoni mwa Waislamu, na havikuhitaji mkusanyiko mkubwa wa kihistoria kama ule wa Ghadir Khum.

Kwa hiyo, kwa mujibu wa Madrasatu Ahlul-Bayt (a.s.), Ghadir Khum ilikuwa ni tangazo la Mwenyezi Mungu kuhusu Wilayah na uongozi wa Imam Ali (a.s.) kwa Umma baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), na si suala la kusisitiza mapenzi na heshima pekee.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha