12 Juni 2026 - 14:40
Khatibu wa Ijumaa Tehran Aonya Marekani na Israel: Mkivuka Mipaka Mtajibiwa kwa Nguvu

Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema Rais Donald Trump na Benjamin Netanyahu watakabiliwa na jibu kali na la uthabiti iwapo wataendelea na uchokozi dhidi ya Iran.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran, Ayatollah Sayyid  Ahmad Khatami, ametoa onyo kali kwa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel, akisema kuwa hatua yoyote ya kuvuka mipaka dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itajibiwa kwa nguvu na uthabiti.
Katika khutba yake ya Ijumaa, Ayatullah Khatami alimlenga Rais wa Marekani Donald Trump pamoja na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu, akisisitiza kwamba endapo wataendelea na vitendo vya uchokozi au kuvuka mipaka yao, watakabiliwa na "jibu kali na la kuumiza."
Amesema Iran haitasita kulinda mamlaka yake, usalama wa taifa na maslahi ya wananchi wake dhidi ya aina yoyote ya uchokozi, akionya kuwa maadui wanapaswa kujifunza kutokana na matokeo ya hatua zao zilizopita.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha