18 Juni 2026 - 23:05
Rais wa Iran Aishukuru Qatar kwa Jukumu Lake la Kupunguza Mvutano na Kuendeleza Diplomasia

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, ameipongeza Qatar kwa mchango wake katika kupunguza mvutano wa kikanda na kuwezesha juhudi za kidiplomasia zilizopelekea kufikiwa kwa makubaliano ya kumaliza vita.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) -ABNA-, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, ameishukuru Serikali ya Qatar kwa nafasi yake muhimu katika kupunguza mvutano wa kikanda na kusaidia kufanikisha njia za kidiplomasia zilizopelekea kufikiwa kwa makubaliano ya kumaliza vita.
 
Rais Pezeshkian alitoa shukrani hizo katika mazungumzo ya simu yaliyofanyika Alhamisi kati yake na Amir wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani. Alisifu juhudi za Doha kwa kuchukua hatua za kuwajibika katika kutuliza hali ya taharuki na kuweka mazingira yaliyowezesha kufikiwa kwa makubaliano hayo.
 

Aidha, Rais wa Iran alieleza kuwa maendeleo hayo yanatoa fursa muhimu ya kupanua ushirikiano wa kikanda, kuimarisha umoja kati ya nchi za Kiislamu, pamoja na kuweka msingi wa amani na utulivu wa kudumu katika eneo.
 
Kwa upande wake, Amir wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, alieleza kuridhishwa kwake na kufikiwa kwa makubaliano ya kumaliza vita, akisisitiza kuwa diplomasia na mazungumzo ndiyo njia bora ya kupunguza migogoro na kuimarisha utulivu wa kikanda.
 

Sheikh Tamim pia alibainisha kuwa tangu kuanza kwa uongozi wa Rais Pezeshkian, Qatar imeendelea kufanya juhudi za kuimarisha uhusiano wake na Iran, sambamba na kusaidia kupunguza mvutano na kusogeza karibu mitazamo ya pande mbalimbali kwa ajili ya kulinda amani na usalama wa eneo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha