Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) –ABNA– Kamanda wa Makao Makuu ya Khatam al-Anbiya (SAW), Meja Jenerali wa Jeshi la Anga Ali Abdullahi, amesisitiza kuwa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vipo katika kiwango cha juu cha utayari kwa ajili ya kuchukua hatua yoyote itakayochangia kuimarisha uadilifu, kulinda haki za wananchi, kukabiliana na vitisho na ufisadi uliopangwa, pamoja na kuimarisha mamlaka na usalama endelevu wa nchi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Makao Makuu ya Vikosi vya Ulinzi vya Iran, Jenerali Abdullahi alitoa kauli hiyo kupitia ujumbe aliomwandikia Mkuu wa Idara ya Mahakama ya Iran, Hujjatul-Islam Ghulam Hussein Mohseni Ejei, kwa mnasaba wa Wiki ya Kitaifa ya Mahakama.
Katika ujumbe huo, Jenerali Abdullahi alieleza kuwa tarehe 7 Tir (sawa na tarehe 28 Juni) ni kumbukumbu ya tukio la kusikitisha na lenye utukufu katika historia ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, ambapo Ayatollah Shahidi Sayyid Muhammad Husaini Beheshti pamoja na watu 72 miongoni mwa wafuasi wa Imam Khomeini (MA) waliuawa shahidi katika shambulio la kigaidi lililolenga makao makuu ya Chama cha Jamhuri ya Kiislamu mwaka 1981.
Alibainisha kuwa damu ya mashahidi hao ilimwagika kwa ajili ya kuimarisha mti wa Mapinduzi ya Kiislamu na kuweka msingi wa uadilifu, utawala wa sheria na ulinzi wa maadili ya Kiungu, huku akilaani vikali kitendo hicho cha kigaidi kilichotekelezwa na kundi la wanafiki.
Your Comment