3 Julai 2026 - 12:15
Hali ya Majonzi Yatanda Tehran sambamba na kuanza kwa Shughuli za Kumuaga Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Hali ya majonzi na huzuni kubwa imeendelea kutawala katika mji wa Tehran kuelekea shughuli za mwisho za kumuaga Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei(Ra), huku umma wa Kiislamu ukiendelea kutoa heshima zake kwa Kiongozi huyu Mwema na mtetezi wa Haki za Wapalestina na Haki za wanyonge popote walipo Ulimwenguni.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Hali ya Majonzi na huzuni kubwa imeendelea kushuhudiwa katika Mji Mkuu wa Iran, Tehran, baada ya kuanza Rasmi shughuli za mwisho za kumuaga Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Hussein Khamenei.

Shughuli hizo za Mazishi zimekusanya wafuasi na wapenzi wa Ahlul-Bayt (as) kutoka maeneo mbalimbali ya nchi ya Iran na Dunia Kwa ujumla, wakionyesha heshima na mshikamano wao katika mazingira ya majonzi na tafakuri ya Kibinadamu na Kiroho.
 
Wachambuzi wanasema kuwa tukio hilo limechukua sura ya kimataifa kutokana na uwepo wa ujumbe mbalimbali na ushiriki wa makundi ya kidini na kijamii yanayoonesha mshikamano na msimamo wa kiongozi huyo katika kuunga mkono haki na harakati za Umma wa Kiislamu.
 
Aidha, mazingira ya mji wa Tehran yameelezwa kuwa na hali ya utulivu pamoja na hisia nzito za majonzi na tafakuri, huku shughuli mbalimbali za maadhimisho zikiendelea kuripotiwa.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha