15 Julai 2026 - 19:18
Afisa wa Lebanon: Makubaliano Mapya na Israel Hayana Uhalali wa Kisheria

Afisa wa Lebanon, Bassam Al-Hashem, amesema kuwa makubaliano ya mfumo yaliyopendekezwa na Israel hayana thamani ya kisheria bila kuidhinishwa na Baraza la Mawaziri na Bunge la Lebanon, akionya kuwa baadhi ya vipengele vyake vinakiuka mamlaka ya taifa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA–, Afisa wa Lebanon, Bassam Al-Hashem, amesema kuwa kile kinachoitwa “makubaliano ya mfumo” kati ya Lebanon na Israel hakina uhalali wa kisheria hadi kitakapopitishwa rasmi na Baraza la Mawaziri na Bunge la Lebanon.

Akizungumza na tovuti ya habari ya Al-Ahed, Al-Hashem alieleza kuwa kutokana na kuwepo kwa nyaraka na makubaliano ya kimataifa yanayotambuliwa tayari, hakuna ulazima wa kuandaliwa makubaliano mapya.

Aidha, alikosoa baadhi ya vipengele vya rasimu hiyo, akisema vinakiuka mamlaka na uhuru wa taifa la Lebanon. Alionya kuwa jaribio lolote la kuifanya Jeshi la Lebanon likabiliane na Harakati ya Muqawama linaweza kuhatarisha umoja wa kitaifa na kuathiri utulivu wa ndani wa nchi hiyo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha