Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Khatibu wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran, Hujjatul Islam Muhammad Jawad Hajj Ali Akbari, amesema kuwa Imam Shahidi Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei (Radhiyallahu 'Anhu) alijitolea kikamilifu katika njia ya Mwenyezi Mungu na akaongoza harakati za mapambano dhidi ya ubeberu wa kimataifa.
Akizungumza wakati wa khutba ya Ijumaa, Hajj Ali Akbari alirejea historia ya harakati za Imam Shahidi kabla na baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, akisisitiza kuwa alichagua njia ya jihadi, subira na kujitolea kwa ajili ya kulinda Uislamu na maslahi ya Umma wa Kiislamu.
Alieleza kuwa msimamo wake thabiti na uongozi wake wa kimapinduzi uliwezesha kuvunja nguvu na ushawishi wa mataifa ya kibeberu yaliyokuwa yakijaribu kuhodhi na kudhibiti hatima ya mataifa mengine.
Khatibu huyo aliongeza kuwa urithi wa Imam Shahidi utaendelea kuwa chachu ya mapambano dhidi ya dhulma, ukandamizaji na ubeberu, huku ukiwahamasisha Waislamu na watu wote wanaopenda haki kusimama imara katika kutetea uhuru, heshima na maadili ya Kiislamu.
Maoni yako