-
Rais wa Misri kwa mara nyingine apinga kuhamishwa Wapalestina Gaza
Rais wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi jana Ijumaa alisisitiza kwa mara nyingine tena kwamba nchi hiyo ya Kiarabu "inapinga kikamilifu" kufurushwa Wapalestina kwenye makazi yao na kuhamishiwa katika nchi nyingine, na kuvitaja vita vya Gaza kuwa "janga la kibinadamu."
-
Du'a Al-Faraj | Jamiat Al-Mustafa (s) - Dar-es-salaam, Tanzania iliyohudhuriwa na Ayatollah "Reza Ramezani" + VIDEO
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Du'a Al-Faraj Reappearance Supplication / Dua ya Al-Faraj (دُعَاء ٱلْفَرَج) - ya kuomba kudhiri kwa Haraka kwa Imam wa Zama (a.r.f.s) iliyosomwa katika Chuo cha Jamiat Al-Mustafa (s) - Dar-es-salaam, Tanzania, ikihudhuriwa na Hojjat Al-Islam wal Muslimin, Ayatollah "Reza Ramezani", Katibu Mkuu Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt (a.s).
-
Sheikh Mtulia katika Darsa la Subhi ya Kimaanawi / Kiroho - Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-es-Salam - Tanzania + Video
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Sheikh Mtulia akitoa Darsa ya Akhlaq / Subhi Maanawi - Subhi ya Kiroho katika Chuo cha Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-es-Salam - Tanzania.
-
Je, Mazungumzo Kati ya Mwanamume na Mwanamke Wasiokuwa Mahramu Yamekatazwa kwa namna yoyote ile katika Uislamu?
“Kauli yenye nguvu zaidi ni hii kwamba kusikia (kusikiliza) sauti ya Mwanamke asiyekuwa Mahram, maadamu si kwa ajili ya tamaa, starehe au maslahi, ni jambo linaloruhusiwa (linajuzu). Vivyo hivyo kwa Mwanamke, ikiwa hakuna hofu ya fitina, anaweza kusikika na Wanaume wasio mahram kwake".
-
Tukio Muhimu la Ufunguzi wa Darul- Qur'an Zainul-A'bidina (a.s) Jijini Mwanza , Tanzania
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Tukio muhimu la ufunguzi wa Darul- Qur'an inayobeba Jina la Zainul - A'bidina (a.s) - Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), limefanyika Jijini Mwanza, Tanzania likisimamiwa na Samahat Sheikh Zaydu Kishama.
-
Afrika Katika Ramani ya Utalii wa Vyakula: Tanzania Yaongoza Jitihada
Tanzania inatazamiwa kuwa mwenyeji wa Kongamano la 2 la Umoja wa Mataifa la Elimu ya Utalii kwa Afrika Mwezi Aprili 2025, likileta pamoja wataalamu wa kimataifa ili kuangazia umuhimu wa utalii wa upishi katika kukuza uchumi na kukuza urithi wa vyakula mbalimbali Barani Afrika.
-
Maandalizi na uhamasishaji wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan 2025 / 1446H - Hawzat Imam Ali (as) Tanga - Tanzania
Hawzat Imam Ali (a.s) iliyopo chini ya Taasisi ya Bilal Muslim Mission Tanga, Tanzania, Kitengo cha uhamasishaji wa Michango ya uwezeshaji wa masira ya Imam Husein (a.s), Leo hii Jumatatu 21/04/2025, kimekutana na Waumini wa Bilal Muslim Bushiri na kuongea nao kuhusiana na Suala la Masira ya Imam Hussein (as) mwaka huu wa 1446H. Lengo la ziara hii, ni kuhamasishana zaidi na kuelezea umuhimu wa kutoa Sadaka hasa katika kuichangia Masira ya Imam Husen (a.s).
-
Habari Pichani | Sherehe ya Kipekee ya Kufikia Umri wa Dini (Taklif) kwa Wasichana wa Karbala
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AhlulBayt (a.s) – ABNA – Sherehe ya bulugh kwa wasichana imefanyika kwa adhama katika mji mtakatifu wa Karbala, Iraq. Takribani wasichana 5,000 kutoka shule 121 walishiriki kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa na Ataba ya Abbasiyya. Tukio hilo lililenga kuwapa wasichana hawa utambuzi wa kidini na kuadhimisha hatua muhimu ya kuingia katika umri wa kuwajibika kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu. Sherehe hiyo imekuwa tukio lenye mvuto mkubwa, likiambatana na hotuba, mawaidha na maombi, na kuwapa washiriki fursa ya kuimarisha uhusiano wao na mafundisho ya AhlulBayt (a.s).
-
Qur'an Tukufu Zanzibar - Tanzania + Video
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Sheikh Ridha Dosa akitoa Somo la Qur'an Tukufu Zanzibar - Tanzania, katika Chuo cha Qur'an Tukufu cha Jamiat Al- Mustafa (s) kinachoongozwa na kusimamiwa na Rais wa Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-es-salaam - Tanzania, Hojjat al-Islam wal Muslimin, Dr.Ali Taqavi.
-
Ujue wajibu wako katika kuiongoza familia yako + Video
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Samahat Sheikh Reihan Yasin, akifafanua mada Muhimu kuhusu mtu kuujua Wajibu wake katika kuiongoza familia yake.
-
Watu waliodhaifu kwako unawatendea vipi? Uislamu unasisitiza kuwatendea watu wema
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as.) - ABNA - Samahat Sheikh Hemed Jalala, Mudir wa Hawzat Imam Sadiuq (a.s) - Kigogo - Post na Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna Ashari Tanzania (T.I.C), amekumbusha umma wa waislamu kuzingatia kuwatendea wema watu hasa wale waliodhaifu, na kuhakikisha kwamba hakuna mtu yeyote anayedhulumiwa na kutendewa ndivyo sivyo. Uislamu unalingania wema na haki kwa watu. Katika maneno yake mafupi na yenye hekima, amesema: "Ukitaka kujua ukweli wa mtu, basi tizama ni jinsi gani anavyowatendea wale waliodhaifu kwake"
-
Ufafanuzi kwa ufupi kuhusiana na hatua za mashindano ya Qur'an Tukufu na Hadithi - Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-es-Salam - Tanzania, 2025
Tangazo la Matokeo ya mwisho litatolewa kuanzia Tarehe 01 - 05 - 2025 mpaka tarehe 05 - 05 - 2025. Na ratiba ya hafla ya fainali ya mashindano haya pamoja na ugawaji wa zawadi kwa washindi na washiriki utakuwa tarehe 17 - 05 - 2025 katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere - Jijini Dar-es-Salam - Tanzania.
-
Maandalizi ya Masira ya Imam Hussein (as) Katika Mwezi wa Muharram - Tanga, Tanzania
Kitengo cha uhamasishaji wa Michango ya uwezeshaji wa masira ya Imam Husein (a.s) - Jumapili ya Leo, sawa na Tarehe 20 /04/ 2024 kimekutana na Waumini wa Bilal Muslim Boza na Bilal Muslim Mjimema.
-
Habari Pichani | Mbebaji wa Qur’an ni Mbeba Bendera ya Uislamu - Mashindano ya Nusu Fainali ya Qur'an Tukufu, Jamiat Al-Mustafa (s) Dar-Es-Salam
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Mashindano ya nusu Fainali ya Qur'an Tukufu yanaendelea Jamiat - Mustafa (s), Dar-es-Salam - Tanzania.Wanafunzi kutoka katika Hawza na Madarisi mbalimbali wanashiriki katika Mashindano haya Matukufu ya Qur'an Tukufu. Shukran za dhati zimwendee Dr. Ali Taqavi kwa kuendelea kusimamia vyema mashindano haya ya Qur'an Tukufu nchini Tanzania, Zanzibar, Burundi na Malawi. Mbebaji wa Qur’an ni Mbeba Bendera ya Uislamu.
-
Habari Pichani | Mzunguko wa Kisomo cha Qur'an Tukufu, Zanzibar - Tanzania
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Rais Mwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-es-salaam - Tanzania, Dr.Ali Taqavi akiwa katika Mzunguko wa Kisomo cha Qur'an Tukufu Zanzibar - Tanzania.
-
Hawzat Imam Ali (a.s) chini ya Bilal Muslim Tanga, Kitengo cha uhamasishaji ilifanya Ziara ya uhamasishaji kwa Waumini wa Bilal Muslim Mwembeni -Tanga
Lengo la ziara hii, kuhamasishana na kuelezea umuhimu wa kutoa Sadaka hasa katika kuichangia Masira ya Imam Hussein (a.s).
-
Habari Pichani | Sala ya Ijumaa Masjid Jamiat Al-Mustafa, Dar-es-salaam - Tanzania
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Leo hii (18 -04- 2025), Sala ya Ijumaa imeswaliwa katika Masjid ya Jamiat Al-Mustafa (s), Dar-es-Salam - Tanzania.
-
Mradi wa Mji wa Wakfu wa Zainabiyyah kutoka Tanzania ukiwa huko Ghaza, umesaidia kukata Kiu ya Wadhulumiwa wa Gaza + Video
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Alhamdulillah, tunayo furaha ya kushiriki pamoja nanyi katika taarifa hii mpya kuhusu Mradi wa Maji wa Wakfu wa Zainabiyya huko Gaza.
-
Habari Pichani | Ziara ya Qur'an Tukufu, Zanzibar - Tanzania iliyofanywa na Sheikh Ridha Dosa chini ya Usimamizi wa Jamiat Al-Mustafa (s) - Tanzania
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Sheikh Ridha Dosa, amefanya ziara maalum Zanzibar - Tanzania iliyoratibiwa na Jamiat Al-Mustafa (s) - Dar-es-salaam - Tanzania kwa ajili ya Qur'an Tukufu. Ni ziara iliyoambatana na Daura fupi kwa Wanafunzi wa Qur'an Tukufu ndani ya Zanzibar - Tanzania. Ziara hii imekuwa ni ziara yenye mafanikio makubwa na Wanafunzi walifaidika zaidi upande wa Qur'an Tukufu.
-
Kikao cha Alhamisi ya Kila Wiki 2025 kwa Wanawake wa Wanaume
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Sifa Muhimu za Mtu Mwenye Mafanikio katika Uislamu. Mada hii inafichua sifa za kimsingi zinazofafanua haiba inayostawi na yenye athari chanya kutoka katika mtazamo wa Kiislamu. Mada hii imewasilishwa siku ya Alhamisi, Aprili 17, 2025, Saa 8:00 - 9:00 PM. Mahali: Haidery Plaza, Ghorofa ya 8, Posta Dar es Salaam, Karibu na Kituo cha Petroli cha GBP. Mzungumzaji: Sheikh Ali Azim Shirazi
-
Habari Pichani | Darul - Qur'an yafunguliwa Jijini Mwanza kwa Jina la Imam Zainul - A'bidina (a.s)
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Tarehe 20 - 04 - 2025, kwa mara ya kwanza itafunguliwa Darul - Qur'an Jijini Mwanza - Tanzania kwa Jina la Imam Zainul - A'bidina (a.s). Sherehe ya ufunguzi wa Shule hiyo ya Qur'an Tukufu itafanyika katika viwanja vya shule hiyo inayopatikana katika katika maeneo ya ILOGANZALA, Mtaa wa Saba Saba. Hafla ya ufunguzi itaanza muda wa saa saba na nusu / 7:30 baada Sala ya Adhuhuri. Wageni mbalimbali wa Taasisi Mbalimbali za Kiislamu wamealikwa katika hafla hiyo, wakiwemo: Viongozi wa Serikali, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, na Bilal Muslim Mission of Tanzania.
-
Al_Itrah Foundation Dar-es-salaam yatoa zawadi ya Qur'an ya Tarjama ya Kiswahili kwa Sheikh Walid Alhad Omar Kawambia, Sheikh wa Mkoa wa Dar-es-salaam
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Leo hii, 17 April 2025, Al Itrah Foundation , Dar-es-salaam - Tanzania imefanya tukio la heshima lililofanyika kupitia Ofisi za Taasisi hii Jijini Dar-es-salaam, ikiwakilishwa na Bw. Khomeini Ruhullah, ambapo ilimkabidhi Sheikh wa Mkoa wa Dar-es-salaam - Sheikh Walid Alhad Omar Kawambia Qur'an Tukufu yenye Tafsiri ya Kiswahili kwa Kalamu ya Marhumu Sheikh Hassan Ally Mwalupa. Zawadi hii muhimu inatambua uzito wa maarifa, mshikamano wa Kiislamu na kiroho.
-
Maandalizi ya Hafla kubwa ya Qur'an Tukufu itakayojumuisha timu mbalimbali za Wasomaji wa Qur'an wa Tanzania, Zanzibar na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul- Bayt (a.s) - ABNA - Dr. Ali Taqavi, Rais wa Jamiat Al-Mustafa (s) yupo katika harakati muhimu za kuandaa Hafla kubwa ya Qur'an Tukufu itakayofanyika nchini Tanzania ikijumuisha Tanzania bara na Zanzibar. Katika picha hizi ni tukio za kukagua na kutembelea uwanja mkubwa wa michezo Jijini Dar-es-Salam - Tanzania, ambao utatumika kwa ajili ya hafla kubwa ya Qur'an Tukufu itakayohudhuriwa na timu kubwa ya wasomaji mahiri wa Qur'an Tukufu kutoka katika nchi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Kipindi cha Nasaha za Ulimwengu | Kwa nini Mwanadamu anafanya Kiburi wakati asili yake ni Maji Machafu?!
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - IBN TV AFRIKA imeendesha na inaendeleza kipindi chake muhimu cha Nasaha za Ulimwengu. Kupitia Kipindi hiki cha "Nasaha za Ulimwengu" Sheikh Ramadhan Masemo ametoa nasaha muhimu kwa Wanadamu na Walimwengu kwa ujumla ambapo ametanguliza swali hili muhimu: Ni kwa nini Mwanadamu anafanya Kiburi wakati asili yake ni Maji Machafu?! Hutamani hata kiyatazama? Sasa kiburi cha nini?!. Kisha akasisitiza katika kunukuu maneno hayo ya Imam Ali (a.s) aliposema: "Mwanadamu unajivunia nini wakati asili yako ni maji machafu? Halafu wewe kama Mwanadamu unatembea na uchafu tumboni?! Na baada ya kufa kwako unageuka na kuwa mzoga unaotoa harufu mbaya sana!" . Sasa kwa nini ujigambe kwa mali, kwa kipaji ulichopewa, uwe na kiburi?. Yote hayo ni mambo yanayopita na tutayaacha hapa hapa duniani.
-
Habari Pichani | Harakati za Kielimu na Kitamaduni Katika Hawza ya Zainul - A'bidina (a.s) - Burundi + Audio
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlu-Bayt (a.s) - ABNA - Hawza ya Imam Zainul - A"bidina (a.s) nchini Burundi inaendelea na harakati zake za Kielimu na Utamaduni wa Kiislamu. Katika picha ni moja ya Harakati za Kielimu na Kitamaduni zinazoendelea kila siku katika Hawza ya Zainul - A'bidina (a.s) - iliyopo Burundi ambapo kila siku Wanafunzi hujipanga katika mistari na kusoma Dua mbalimbali za kila siku, katika picha ni tukio la kusoma Dua ya Siku ya Alkhamisi (kama inavyoonekana hapo chini katika Maandidhi na Audio kwa sauti ya Aba Dhar Al-Halawaji).
-
Chuo Kikuu cha Jamiatul Mustafa - Dar-es-salaam - Tanzania kimeandaa Kongamano la Kisayansi kuhusu Maendeleo katika Ulimwengu wa Kiislamu
Kongamano hili litajadili juu ya Maendeleo katika Ulimwengu wa Kiislamu kati ya changamoto na mkakati. Mhadhiri: Samahat Sheikh Mulaba Saleh. Siku ya: Jumamosi; 19/04/2025. Kuanzia: 10 - 12:00 AM. Katika Ukumbi wa Sala wa Chuo cha Jamiat Al- Mustafa. Watu wote mnakaribishwa kuhudhuria katika nad'wa hii ya Kisayansi.
-
Mufti wa Tanzania atangaza Dua ya Kuiombea Nchini na Wazee waliotangulia mbele ya Haki | Rais Samia Hassan na Rais Mwingi Kushiriki
Dua ya Kuiombea Taifa la Tanzania na kuwarehemu Wazee wetu waliotangulia mbele ya Haki itaongozwa na Mheshimiwa Mufti wa Tanzania.
-
Habari Picha + Video | Wanafunzi wa Hawzah ya Hazrat Zainab (sa) wakijishughulisha na Kilimo / Kilimo ni UTI wa Mgongo wa Uchumi wetu
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Mabanati wa Hawzah ya Hazrat Zainab (amani iwe juu yake), wakiwa katika hali ya kujishughulisha na kazi ya Kilimo. Kila mmoja wao katika kundi la watu watatu, anamiliki kipande cha ardhi. Wanalima na kupanda mazao yao, na wakati wa kuvuna, sisi (Uongozi wa Jamiat Al-Mustafa - Dar-es-salaam, Tanzania) tunanunua mavuno / bidhaa hizo kutoka kwao. Kilimo ni UTI wa Mgongo wa Uchumi wetu. Hivyo tufikiri zaidi na kuwaza katika Kilimo. Tujaribu kufanya Kilimo hata kwa kiasi kidogo.
-
Sikiliza Utamu wa Qur'an Tukufu! | Kwa Hakika Qur'an Tukufu ni Tabibu Mkuu wa Nyoyo + Video
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Sikiliza utamu wa sauti inayokariri Kurani Tukufu! Hakika Qur'an Tukufu ni Tabibu Mkuu wa Nyoyo.
-
Kozi ya Kompyuta kwa Vitendo ya ICDL kwa Wanafunzi wa Hawzat Sayyidat Zainab (s.a) - Jamiat Al-Mustafa, Dar -es- Salaam - Tanzania
ICDL inawakilisha Leseni ya Kimataifa ya Fani ya (Computer) Kompyuta. Na hiyo ndio maana ya Kozi hii ya ICDL - Yaani: International Computer Driving License. Hii ni Kozi muhimu katika Kozi za Kompyuta ambazo zinauwezo wa kumsaidia na kumsapoti mtu yeyote kujikwamua Kiuchumi.