Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-, Kamati ya Uratibu ya Makundi ya Muqawama ya Iraq imetangaza katika msimamo wake kwamba: Asili ya uhusiano kati ya Iraq na Marekani haikujengwa juu ya msingi wa usawa kati ya nchi mbili huru; kwa sababu Washington bado inaingilia mambo ya ndani ya Iraq na hata inaamua ni sura zipi za kisiasa ziruhusiwe kushika nyadhifa za kiserikali na ni nani aondolewe; na hilo hufanyika kwa kuzingatia matakwa ya Marekani na ndani ya mkabala unaofuatwa katika sera zake za kutawala na kujitanua.
Kamati hiyo imeongeza: bila shaka wavamizi bado wanaendelea kukiuka anga la Iraq; iwe kupitia ndege zisizo na rubani (drones) au kwa kutumia ndege zao za kivita. Hatua hizi ni tishio kubwa kwa usalama, uthabiti na umoja wa ardhi ya nchi, na ni uvamizi wa wazi dhidi ya mamlaka na heshima ya dola ya Iraq.
Kamati ya Uratibu imesisitiza: Sisi katika Muqawama wa Iraq tunathibitisha kwamba Marekani haijatekeleza kikamilifu ahadi zake zote, na hatujaona hatua yoyote ya kweli ya kutekeleza vipengele vilivyosalia vya makubaliano na serikali ya Iraq vinavyosisitiza kuondoka kikamilifu kwa majeshi yote ya kigeni kutoka ardhi na anga ya Iraq. Msisitizo huu wa kuchelewesha mambo na kukwepa majukumu unatulazimisha kubeba wajibu wetu wa kisharia na kimaadili katika kuchukua misimamo inayolingana na hadhi ya taifa letu na haki yake halali ya kumaliza uvamizi; iwapo wao wataendelea kung’ang’ania kubaki na kulazimisha matakwa yao juu ya nchi.
Your Comment