Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo inaadhimisha kumbukumbu ya kuuawa shahidi kwa Mostafa Chamran, mmoja wa viongozi mashuhuri wa kisiasa na kijeshi ambaye alitoa maisha yake tarehe 21 Juni wakati wa vita vilivyoanzishwa na Iraq dhidi ya Iran kati ya mwaka 1980 na 1988.
Kwa mujibu wa kauli ya Ali Khamenei, Dkt. Chamran alikuwa mwanasayansi aliyekuwa na maisha mazuri nchini Marekani, lakini aliacha mafanikio hayo na kurejea Mashariki ya Kati ili kuwatetea waliodhulumiwa na kushiriki katika harakati za Mapinduzi ya Kiislamu na ulinzi wa Iran.
Safari ya maisha ya Shahidi Chamran imekuwa ikitajwa kuwa ilianzia katika masomo na utafiti nchini Marekani, ikiwemo katika Jimbo la Texas, hadi kufika mstari wa mbele wa mapambano huko Dehlavieh, ambako aliuawa shahidi akiwa mstari wa mbele akitetea nchi yake.
Kumbukumbu ya Shahidi Mustafa Chamran huadhimishwa kila mwaka nchini Iran kama ishara ya kujitolea, uzalendo na kujitoa mhanga kwa ajili ya kutetea haki na taifa.
Your Comment