-
Habari Pichani | Usomaji wa Qur'an Tukufu katika Mji wa "Tal Afar" nchini Iraq
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - Abna - Ibada ya kusoma sehemu ya Qur'an Tukufu hufanyika kila siku wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na juhudi za Haram ya Maimamu wawili al-Askariyyayni (aamani iwe juu yao) katika Msikiti wa Imam Hakim, katika Mji wa "Tal Afar", katika Mkoa wa Nainawa, Kaskazini mwa Iraq.
-
Ripoti ya Picha | Mkutano wa Nowruz baina Ayatollah Ramezani na Wafanyakazi wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahl al-Bayt (AS) huko Qom - Iran
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (A.S) - Abna - Ayatollah Reza Ramezani, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahl al-Bayt (A.S) amekutana na Wafanyakazi Kitengo cha Kisayansi na Utamaduni wa Jumuiya hii katika Mji wa Qom kabla ya adhuhuri ya leo, Jumatano, Machi 26, 2025, ikiwa ni mwanzoni mwa Mwaka Mpya wa 1404 Hijria - Shamsia.
-
Ahkam za Kisheria kwa Mujibu Ahlul-Bayt (a.s):
Hukumu za Kisheria zitakazomfanya Mwanadamu afaulu Kesho Siku ya Kiyama
Hukumu za Kiislamu zinakutaka Muislamu Itikadi yako iwe ni Itikadi sahihi. Na Uislamu unatufndisha kuwa haijuzu kwa Muislamu yeyote kumfuata (Kumqalid) mtu kuhusiana na suala la Kiitikadi, kwa maana kwamba: Lolote linalohusiana na itikadi, inabidi Muislamu ulikubali na kuliitikadia kwa kutegemea dalili na uthibitisho madhubuti ima wa: Qur’an Tukufu, au Hadithi na Sunna za Mtume (Rehma na amani ziwe juu yake na Aali zake) na Riwaya mbalimbali za Maimam watoharifu (amani iwe juu yao), au uwe ni uthibitisho unaotokana na dalili za kiakili.
-
Habari Pichani | Qur'an ni Nuru, na ni Kiongozi Bora wa Maisha yetu | Mashindano ya Qur'an Hawzat Al-Qaim (a.s), Tanga Tanzania
Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s); Bilal Muslim Tanga Mjini imefanya Mashindano ya Qur'an Tukufu katika vipengele :Taj'wid, Tartili, Hifdhi Juzuu 15, na Juzuu 5, na Juzuu 2, na Juzuu 1. Mashindano yalijumuisha Maarif al-Qur'an (Tafsiri ya Surat Al-Hujurat, na Surat AI-Insan). Washiriki katika mashindano hayo ni: Wanafunzi (Wavulana) wa Hawzat al-Qaim (atfs), Wanafunzi (Wasichana) wa Hawzat Al-Zahra (s.a), Waumini (jinsia zote), Wanafunzi wa Madrasa (jinsia zote). Pia mashindano hayo yamehudhuriwa na wageni mbali mbali wakiwemo viongozi wa Serikali na Kidini. Shukran za dhati ziende kwa Mudiru wa Hawza,Samahat Sheikh Kadhim kwa kupangilia na kufanikisha mashindano haya. Pia shukran za dhat ziende kwa uongozi wa Bilal Muslim Tanga Mjini kwa kujitolea kwa hali na mali kuhakikisha mashindano haya ya Quran Tukufu yanafanyika. Qur'an ni nuru, na ni Kiongozi wa Maisha yetu.
-
Kuangalia aina za "Istikhara" kwa mujibu wa Mtazamo wa Riwaya
Istikhara ni dhana (mafhumu) ya kidini ambayo ina (maana au) ufafanuzi wake na aina zake katika vyanzo vya kidini.
-
Oxfam: Israel imegeuza njaa kuwa silaha ya vita/dunia inashiriki katika jinai Gaza kwa kunyamaza kimya
Sambamba na kushtadi mashambulizi ya anga na nchi kavu ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza; Shirika la Kimataifa la Oxfam limetangaza katika ripoti yake kuwa Israel kwa mpangilio maalumu inatumia njaa kama silaha ya vita dhidi ya raia wasio na hatia wa eneo hilo.
-
China yaitaka Syria iunde serikali shirikishi na ipambane na ugaidi
Mwakilishi wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa amewataka viongozi wa mpito wa Syria waandae mchakato wa kuasisi serikali shirikishi na wachukua hatua madhubuti za kupabana na ugaidi nchini humo.
-
Takriban watu 1,400 wametiwa mbaroni huku maandamano yakiendelea Uturuki licha ya kupigwa marufuku
Mamlaha husika nchini Uturuki zimewatia mbaroni waandamanaji zaidi ya 1,400 huku maandamano ya mitaani yakiendelea kushuhudiwa katika miji mikubwa ya nchi hiyo kupinga marufuku ya kuandamana kufuatia kufungwa jela Meya wa mji wa Istanbul, Ekrem Imamoglu kwa tuhuma za ufisadi, kuongoza genge la uhalifu, utovu wa nidhamu na mengineyo.
-
HAMAS: Uvunjeni mzingiro, komesheni mauaji na hitimisheni kuteswa Wapalestina kwa njaa
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imetoa taarifa ya kulaani "mauaji ya kutisha" yanayoendelea kufanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel na kuitolea mwito Jamii ya Kimataifa ichukue hatua za kuudhibiti utawala huo dhalimu.
-
Makumi ya wafanyakazi wa UN wanaondoka Gaza, Israel yazidisha mauaji
Kufuatia mashambulizi ya Israel dhidi ya kambi za Umoja wa Mataifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na kuuawa wafanyakazi watano wa shirika hilo la kimataifa, makumi ya wafanyakazi wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa katika Ukanda wa Gaza wanaondoka eneo hilo kutokana na wasiwasi wa mashambulizi ya Israel.
-
Mapatano na Lebanon; ndoto ya Wazayuni na upinzani mkali wa Walebanon
Nabih Berri, Spika wa Bunge la Lebanon amefichua mpango wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kutaka kuiburuza nchi hiyo ya Kiarabu katika mtego wa kuanzisha nayo uhusiano wa kawaida, na kusisitiza kuwa, Lebanon katu haiko tayari kuwa na uhusiano wa aina hiyo na utawala huo.
-
HAMAS: Netanyahu anaongopa akidai vita vitawarejesha mateka wote wakiwa hai
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imemshutumu Waziri Mkuu wa Israel, Benjami Netanyahu kwa "kudanganya familia za [mateka], anapodai kuwa chaguo la kijeshi lina uwezo wa kuwarejesha (mateka wote) wakiwa hai."
-
Iran: Wakimbizi wa Afghanistan watarejeshwa kwao kwa heshima
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, viongozi wa Iran na Afghanistan wameandaa utaratibu mzuri wa pamoja wa kuwawezesha wakimbizi wa Afghanistan waliopo nchini Iran warejee nchini kwao kwa heshima.
-
Qaarii wa kimataifa wa Iran asoma kisomo cha Qur'ani kwenye mikesha ya Lailatul-Qadr, China
Kwa ushirikiano wa Ubalozi mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mji wa Guangzhou na Ofisi ya Mwambata wa Utamaduni katika mkuu Beijing, Adnan Momineen, msomaji mashuhuri wa kimataifa wa Qur'ani Tukufu kutoka Iran ameshiriki na kusoma Qur'ani katika ibada za mikesha ya Lailatul-Qadr mjini Guangzhou.
-
Iran yazionya nchi jirani: Jihadharini na ufitinishaji na ufarakanishaji wa Marekani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia tuhuma zilizotolewa na viongozi wa Marekani kuhusiana na kuiwekea mashinikizo Iran na akasema: "inavyotarajiwa, nchi jirani na marafiki zitajihadhari na ufitinishaji na ufarakanishaji unaofanywa na Marekani".
-
'Mauaji makubwa zaidi ya watoto': Iran yalaani mauaji ya Israel na US dhidi ya watoto wa Gaza
Jamhuri ya Kislamu ya Iran imelaani vikali mauaji ya halaiki ya utawala wa Israel dhidi ya watoto wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza, na kuyataja kuwa ni sehemu ya sera ya iliyopangwa ya mauaji ya kimbari yenye lengo la kufuta utambulisho wa Wapalestina.
-
Kashfa ya usalama wa Marekani; taarifa nyeti za kijeshi kuhusu Yemen zavuja
Kosa kubwa la utawala wa Trump katika kutumia mtandao usio na usalama kabla ya kuishambulia Yemen limezusha wimbi la wasiwasi katika duru za kisiasa na kijasusi za nchi hiyo.
-
Iran yazindua ‘Mji Mkubwa wa Makombora’ chini ya ardhi
Kikosi cha Anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) kimezindua “mji mkubwa wa makombora" ulioko chinia ya ardhi, ukiwa ni moja kati ya vituo vyake vingi vya aina hiyo.
-
Vyombo vya Habari na kuhalalisha uchokozi wa utawala wa Kizayuni / Kutoka Mlima Hermoni huko Syria hadi kilele cha juu kabisa cha Israeli!
Baada ya kuporomoka kwa utawala wa Bashar al-Assad, utawala wa Kizayuni ulipanua maendeleo yake na kuteka maeneo zaidi ya Syria. Mojawapo ya shabaha kuu za maendeleo haya daima imekuwa Mlima Hermon, wenye urefu wa kimkakati ambao una nafasi maalum katika milinganyo ya kijeshi ya eneo hilo.
-
Ripoti ya Picha | Mikusanyiko ya Jioni (Alasiri) ya Qur'an katika Bustani za Qom
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna - Sambamba na Siku za Baraka za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ikiwa ni kwa mwaka wa tano mfululizo, na kupitia juhudi za kikundi cha Tablighi cha Jihadi cha Shahidi Muhammad Reza Shafi'i, mikusanyiko ya duru za usomaji wa Qur'an Tukufu zinazohudhuriwa na wanaumena wanawake wanaofunga saumu ya Ramadhani, zimekuwa zikifanyika katika Bustani, bila kusahau uwepo wa watoto na vijana, ambapo huambatana na programu maalum zinazojiri katika Bustani hizo, katika Mji wa Qom. Program hii inaendelea hadi mwisho wa Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan. Bustan kama vile: Narges (Mji mdogo wa Mahdiyeh wa Wanafunzi), Saba (Nirugah, Javad Al-Aimeh), Taravat (Pardisan), Ostad Shahryar (Nirugah), Haram ya Mashahidi wa Mlima wa Khidhri Nabi (amani iwe juu yake), Shahid Mahmoodabadi (Tavanir), Shahidi Shahid Bun'yadiy (Khakfaraj), Nukhbogan (Pardisan), Hafez (Nirugah), Hashemi (Bajek), Banafsheh (Barabara ya Shahid Karimi) na Shahidi Zeinuddin (Bon'yad), zinajumuishwa katika mpango wa kufanya mikutano na mikusanyiko ya enzi ya Qur'an katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani 2024 - 2025.
-
Video | Kikosi cha Jeshi la Wanaanga cha IRGC Kimezindua Mji wa Makombora ya Uhakika
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (AS) - Abna -; Kikosi cha Jeshi la Wanaanga cha Iran (IRGC) kimezindua mji mpya kabisa (wa chini ya ardhi) ambao ni mojawapo ya miji yake ya Makombora ya uhakika. Mji huu mpya wa Makombora uliozinduliwa leo hii, umesheheni aina zote za Makombora ya Khaybar Shekan, Haji Qasim, Qadr H, Sejjil, Emad na Kombora la Cruise la Paveh
-
Qur'an ni Msingi wa Maisha yetu, na ni Kitabu cha kweli, chenye kudumu milele
Muislamu mwenye kuhifadhi Qur'an Tukufu na mwenye Elimu juu ya Qur'an Tukufu, huyo atakuwa ni mwenye kuangaziwa na Nuru ya Qur'an kaburini mwake, na Mtume Muhammad (s.a.w.w) atakuwa Shahidi wake kesho Siku ya Kiyama.