-
Ripoti Pichani | Programu Maalum za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani zinazohudhuriwa na Mashia nchini Tanzania
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (AS) - Abna -; Programu maalum za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani zinafanyika katika vituo 11 vya Kidini nchini Tanzania kwa kushirikisha Mashia wa nchi hii chini ya Ufadhili wa Taasisi ya Hojjatul- Asr (a.t.f.s) ya Tanzania. Miongoni mwa programu hizo maalum ni Kusoma Qur'an Tukufu, Kusoma cha Dua ya Iftitah, Kikao Maalum cha Tafsiri ya Qur'an, Muhadhara wa Kimadhehebu, Kusimamisha Sala ya Jamaa, na kushiriki kwa pamoja katika Meza ya Iftar.
-
Rekodi nyingine kwa Israeli; Gaza ina watoto wengi waliokatwa viungo katika historia!
Gaza ina idadi kubwa zaidi ya watoto waliokatwa viungo vyao katika historia ya kisasa, huku Israel ikizidisha mzozo wa kibinadamu kwa kukiuka usitishaji vita na mzingiro.
-
Hazrat Ayatollah Javadi Amoli:
Siku ya Quds ni sehemu ya "Siku ya Kimataifa ya Uislamu"
Ayatollah Javadi Amoli, akiwaalika watu kushiriki katika Maandamano ya Siku ya Quds, alisema: Ni wajibu wetu sote kushiriki katika Maandamano haya, kwanza, Na kila mmoja wetu kwa mujibu wa elimu tuliyo nayo, awe na nia ya Tawalli na Tabarri ya Kimungu, pili, na kujaribu kufayanya kuwa maandamano mapana zaidi, tatu, yaani tuyafanye maandamano haya kwa nia ya kuwa karibu na kuwaheshimu na kuwathamini Mashahidi wa njia hii, ili hatua hizi zote zithibitishwe na Dhati Takatifu ya Mwenyezi Mungu.
-
Siku ya Quds Duniani:
Amani ya Palestina, ni Amani ya Tanzania
Wito wa kujitokeza kwa watu wote, Waislamu na Watanzania wote wapenda Haki katika siku ya Kimataifa ya Quds, ili kuungana na Wapalestina katika kutetea Haki zao za Kibinadamu katika Taifa lao la Palestina, na vile yakiwa ni Matembezi ya Masjid Al_Aqsa, ambayo ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu.
-
Jeshi la Israel lamuua Msemaji wa HAMAS katika muendelezo wa mauaji ya kimbari Ghaza
Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limemuua shahidi Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS Abdel-Latif al-Qanoua, katika shambulio la kigaidi usiku wa manane wa kuamkia leo lililolenga eneo la Jabalia kaskazini, katika Ukanda wa Ghaza.
-
Licha ya vizuizi vya Israel Wapalestina 180,000 wamesali Msikiti wa Al-Aqsa mkesha wa Lailatul-Qadr
Waislamu Wapalestina wapatao 180,000 walisali Sala ya Tarawehe katika Msikiti wa Al-Aqsa mjini Baitul-Muqaddas usiku wa kuamkia leo na kujiandaa kwa mkesha wa mwezi 27 Ramadhani unaokadiriwa kwamba unaweza ukawa ni Lailatul-Qadr, licha ya vizuizi vikali walivyowekewa na utawala wa Kizayuni wa Israel vya kuingia msikitini humo.
-
Hamas yataka walimwengu wajitokeze kwa wingi kuiunga mkono Palestina Siku ya Quds
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas imetoa mwito wa kuhamasishwa walimwengu kujitokeza kwa wingi katika siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili ili kuonyesha mshikamano na Gaza na al-Quds wakati huu ambapo Israel, kwa uungaji mkono wa Marekani, inaendelea na vita vyake vya mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina Gaza, mkabala wa kimya cha dunia.
-
Kaulimbiu ya Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu ni Tuko kwenye Ahadi Ewe Quds
Mkuu wa Kamati Kuu ya Intifadha na Siku ya Kimataifa ya Quds amesema kuwa: Tutaadhimisha Siku ya Quds mwaka huu kwa kaulimbiu ya Tuko kwenye Ahadi Ewe Quds ikiwa ni kumbukumbu ya shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, shahidi Haniyeh na makumi ya mashahidi wa kambi ya Muqawama.
-
Bahraini, ambaye alikuwa akizungumza katika kikao kilichofanyika katika Makao Mkauu ya Umoja wa Mataifa kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Kupmabana
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran, Esmaeil Baghaei amemkosoa vikali mkuu mpya wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas, kutokana na matamshi yake ya karibuni ya kuitaja Iran kama "tishio" wakati wa ziara yake ya karibuni katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na Israel.
-
Balozi wa Iran akosoa kuenea chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi
Ali Bahraini, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva, amekosoa kuenea kwa chuki dhidi ya Uislamu au kwa maneno mengine Islamophobia katika nchi za Magharibi
-
Siku ya Quds, Jihadul Islami yasisitiza: Muqawama bado una nguvu
Ziad Al-Nakhala, Katibu Mkuu wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina ametoa hotuba kwa mnasaba wa maandalizi ya Siku ya Kimataifa ya Quds akiwapongeza mashahidi wa Operesheni Kimbunga cha al Aqsa na kusema: "Malengo yetu ni ya hali ya juu na adhama yetu ni kubwa. Wazayuni wauaji na washirika wao hawawezi kuvunja irada yetu, na tunazidi kuwa na nguvu. Muqawama wetu unaweka historia isiyosahaulika leo hii."
-
Kutozwa ushuru wa asilimia 25 na Marekani kwa nchi zinazonunua mafuta ya Venezuela
Rais Donald Trump wa Marekani ametangaza kutoza ushuru wa asilimia 25 kwa biashara yoyote na nchi zinazonunua mafuta na gesi ya Venezuela. Ameelezea ushuru huu kama jibu la kutumwa Marekani wanachama wa genge la uhalifu la "Tren de Aragua".
-
Trump asaini amri ya kubadilisha mfumo wa uchaguzi na upigaji kura Marekani, apingwa vikali
Rais wa Marekani Donald Trump amesaini amri ya kiutekelezaji ya kubadilisha mfumo wa uchaguzi na upigaji kura wa nchi hiyo, inayojumuisha sharti la uthibitisho wa uraia kwa usajili wa wapiga kura.
-
Ndege za kivita za Trump haziwezi kuipigisha magoti Yemen
Chombo kimoja cha habari cha Marekani kimeandika makala ya uchambuzi na kusema kuwa, mashambulizi ya kijeshi ya Marekani, Israel na washirika wao kamwe hayawezi kulipigisha magoti taifa la Kiislamu la Yemen.
-
Rais Pezeshkian: Taifa la Iran linapaswa kuonyesha umoja katika Siku ya Kimataifa ya Quds
Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa wito kwa wananchi wa Iran kuonyesha umoja na mshikamano wao wakati wa Siku ya Kimataifa ya Quds, akisisitiza kwamba kujitokeza kwa wingi wananchi katika siku hii kutaonyesha msaada usiotetereka wa Jamhuri ya Kiislamu kwa malengo ya ukombozi wa Palestina.
-
Mkuu wa Kikosi cha Quds: Iran itaendelea kuwa bega kwa bega na Palestina kwa operesheni za kijeshi
Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko thabiti katika msimamo wake wa kuunga mkono kadhia ya Palestina kupitia uungaji mkono wa moja kwa moja kwa vikosi vya Muqawama na kwa operesheni za kijeshi kama zile za Ahadi ya Kweli.
-
Iran, Lebanon, Iraq, Yemen zaanza luteka ya kuwanga mkono Wapalestina Gaza
Vikosi vya Baharini vya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) pamoja na vikosi kutoka Lebanon, Iraq na Yemen, vinafanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya majini katika 'maonyesho ya nguvu' dhidi ya Israel na kutangaza mshikamano na Wapalestina huko Gaza.
-
Iran imefuzu kwa ajili ya Kombe la Dunia 2026
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-; Wakati wa kujivunia kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran🇮🇷baada ya kufuzu kwa ajili ya Kombe la Dunia la 2026. Hii ni mara ya 7 kwa Iran kufuzu kwa ajili ya michuano hiyo ya Kombe la Dunia. Ushindi huu umepatikana katika Mechi ya Siku ya Jumanne baada ya Mehdi Taremi kufunga mabao mawili kipindi cha pili na kuifanya timu yake kutoka sare ya 2-2 na Uzbekistan kwenye Uwanja wa Azadi Mjini Tehran katika Mchujo wa Kundi A la Asia.
-
Gwaride la Boti 3,000 za Kijeshi za Iran litafanyika kuwaunga Mkono Wananchi wa Palestina
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran limetangaza Gwaride la Boti za Kijeshi 3,000 na uhamasishaji wa Wananchi kwa ajili ya kuwaunga mkono Wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.
-
Ayatollah Makarem Shirazi:
Maandamano ya Siku ya Quds ni Nguvu ya Moyo kwa Mujahidina na Wanyonge wa Palestina na Lebanon
Ayatollah Makarem Shirazi, Miongoni mwa Marjii Taqlid, amewaalika Waislamu ili kushiriki katika Maandamano ya Siku ya Quds, alifafanua akisema: Ni muhimu kwa viongozi na marais wa nchi za Kiislamu kuazimia na kuhakikisha azma yao ya kuacha kutojali na kupuuzia jinai za Wazayuni.
-
Njia ya Dhambi Huanza na Dakika ya Uzembe
Tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie sote tupate taufiki ya kushikamana na Ahlul-Bayt (a.s) wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), kwani wao ndio Njia iliyonyooka, na atakayeshikamana nao wao na Qur'an Tukufu, huyo ataepukana na upotevu, kwa sababu wao ndio sehemu ya Kizito cha pili baada ya Qur'an Tukufu, na Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) ametuusia katika Hadithi Sahih na Mutawatiri ya Thaqalayni, kushikamana na Ahlul-Bayt (a.s) na Quran Tukufu ili tuje kupotea baada yake.