-
Habari Pichani | Kozi ya Kompyuta kwa Vitendo ya ICDL kwa Wanafunzi wa Hawzat Sayyidat Zainab (s.a) - Jamiat Al-Mustafa, Dar -es- Salaam - Tanzania
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Jamiat Al-Mustafa, Dar -es- Salaam - Tanzania, Chini ya Usimamizi na Uongozi wa Hojjat Al-Islam wal - Muslimin, Dr. Ali Taqavi, inaendesha Kozi muhimu ya Kompyuta kwa Vitendo ya ICDL kwa Wanafunzi (Mabanati) wa Hawzat Sayyidat Zainab (s.a). Kozi hii inayoboresha ujuzi wa ICDL ni moja ya harakati muhimu za Kielimu na Maarifa kwa Mabanati wa Kiislamu wanaosoma katika Hawzat hii.
-
Kozi ya Kompyuta kwa Vitendo ya ICDL kwa Wanafunzi wa Hawzat Sayyidat Zainab (s.a) - Jamiat Al-Mustafa, Dar -es- Salaam - Tanzania
ICDL inawakilisha Leseni ya Kimataifa ya Fani ya (Computer) Kompyuta. Na hiyo ndio maana ya Kozi hii ya ICDL - Yaani: International Computer Driving License. Hii ni Kozi muhimu katika Kozi za Kompyuta ambazo zinauwezo wa kumsaidia na kumsapoti mtu yeyote kujikwamua Kiuchumi.
-
Vita vya ushuru kati ya Marekani na China: Beijing kukabiliana na ubabe wa Washington
Rais Xi Jin Ping wa China amesisitiza katika mazungumzo na Pedro Sanchez, Waziri Mku wa Uhispania ulazima wa kuimarisha ushirikiano kati ya China na Umoja wa Ulaya ili kukabiliana na hatua za upande moja za Marekani.
-
Washington Post: Ushuru wa kihistoria wa Trump kwa China unaathiri uchumi wa Marekani na dunia
Gazeti la Washington Post limeandika kuwas: Athari za ushuru wa kihistoria uliowekwa na Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya China zimeenea zaidi ya Marekani na kuathiri uchumi wa dunia.
-
CNN: Uvumilivu wa Wamarekani kwa Tel Aviv unaisha
Chanzo makini kimetangaza kuwa, subira ya Wamarekani kwa vitendo vya utawala wa Kizayuni wa Israel inakwisha.
-
Watetezi wa haki za binadamu wa Marekani wafungua kesi kusitisha vikwazo vya Trump dhidi ya maafisa wa ICC
Watetezi wa haki za binadamu wa Marekani wamewasilisha kesi mahakamani ili kusimamisha amri ya utendaji ya Rais Donald Trump ya kumwekea vikwazo Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), wakisema inakiuka vipengengee vya katiba kuhusu haki zao za uhuru wa kujieleza.
-
Ripoti: EU inakabiliwa na mgogoro wa afya ya akili ya vijana
Mgogoro wa afya ya akili kwa vijana katika nchi za Umoja wa Ulaya (EU) unazidi kuongezeka. Mjadala katika Bunge la Ulaya umebaini kuwa asilimia 20, ambayo ni sawa na vijana milioni 14, sasa wanahangaika na matatizo ya kisaikolojia.
-
Nakala adimu ya Qur’ani katika Msikiti wa Al-Aqsa, iliandikwa na mjukuu wa Mtume
Jumba la Makumbusho ya Kiislamu katika Msikiti wa Al-Aqsa, Quds Tukufu (Jerusalem) inayokaliwa kwa mabavu, lina idadi ya vitabu adimu, ikiwa ni pamoja na nakala ya kipekee ya Qur’ani iliyoandikwa kwa hati za Kufi, ambayo mwisho wake inaeleza kuwa iliandikwa na Al-Hasan bin Al-Hussen bin Ali bin Abi Talib (as), mjukuu wa Mtume Muhammad, (saw).
-
Hamas: Shambulio la Israel katika Hospitali ya Kibaptisti ni uhalifu wa kivita kwa msaada wa Marekani
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesema kuwa, kulipuliwa kwa Hospitali ya Kibaptisti katika mji wa Gaza, kuharibiwa jengo la mapokezi na huduma za dharura na kutimuliwa wagonjwa na majeruhi ni uhalifu mpya wa kivita uliofanywa na jeshi la Israel kwa baraka za Marekani ikiwa ni sehemu ya uhalifu wa kikatili unaoendelea kufanywa katika Ukanda wa Gaza.
-
Taasisi ya Palestina: Jamii ya kimataifa isaidie sekta ya afya na tiba ya Gaza
Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imelaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel kwa kuishambulia Hospitali ya Al Maamadani na kuitaka jamii ya kimataifa kuisaidia sekta ya afya na tiba ya eneo hilo.
-
Waislamu wauawa India katika maandamano ya kupinga Sheria ya Marekebisho ya Wakfu wa Kiislamu
Watu watatu, akiwamo mtoto mmoja, wameuawa na wengine zaidi ya 100 kukamatwa wakati wa maandamano yaliyofanyika katika jimbo la mashariki mwa India la West Bengal kupinga marekebisho ya Sheria ya Bodi za Wakfu wa Kiislamu.
-
Jamii ya kimataifa yaendelea kunyamazia kimya jinai za Israel
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limetoa onyo kali kuhusu vifo vya watoto wa Gaza kwa wingi kutokana na njaa kali na ukosefu wa chakula.
-
Wizara: Iran imezalisha mifumo ya ulinzi zaidi ya 900
Wizara ya Ulinzi ya Iran imesema sekta ya ulinzi ya Jamhuri ya Kiislamu imeunda zaidi ya mifumo 900 ya ulinzi na zana za kijeshi; hatua inayoashiria ustawi wa kiwango kikubwa ikilinganishwa na kipindi cha kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979.
-
-
Iran yaitaka UN kutumia uwezo wake kusitisha mauaji ya kimbari Ukanda wa Gaza
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameuhimiza Umoja wa Mataifa kutumia uwezo wake wote kusimamisha mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza na mashambulizi yake dhidi ya watu wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Iran: Tunafanya mazungumzo na Marekani kuhusu kadhia ya nyuklia tu
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, tunapoangalia mawasiliano ya maandishi yaliyofanyika tangu mwanzo wa mchakato uliopelekea kufanyika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati yetu na Marekani tutaona kuwa, msingi wa mawasiliano hayo haukuwa na chochote kingine ghairi ya suala la nyuklia.
-
Kiongozi Muadhamu: Adui amekatishwa tamaa na ana hofu na maendeleo ya Jamhuri ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Sayyid Ali Khamenei leo Jumapili mchana amekutana na baadhi ya makamanda wa jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mnasaba wa Mwaka Mpya wa Kiirani wa Hijria Shamsia na kusisitiza kuwa, adui amekata tamaa vibaya na amekasirishwa na maendeleo ya Jamhuri ya Kiislamu. Wakati huo huo amesisitiza kwamba, pamoja na kuwepo mapungufu, lakini kuna maendeleo pia yamepatikana, inabidi hayo nayo tuyaone.
-
Habari Pichani | Tamasha la 30 la Kimataifa la Al-Mustafa la Qur'an na Hadithi - Zanzibar, Tanzania
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Tamasha la 30 la Kimataifa la Al-Mustafa la Quran na Hadithi - Zanzibar, limefanyika kwa mafanikio makubwa chini ya uongozi na usimamizi wa Mwakilishi wa Jamiat Al-Mustafa, Tanzania - Dr. Ali Taqavi. Wanafunzi wa Jamiatul-Mustafa - Tanzania na vyuo vingine wameshiriki katika Mashindano haya ya Hifz ya Quran Tukufu na Hadithi. Hii ni katika kuhuisha utajo wa Quran Tukufu na hii ni harakati muhimu ya kuthamini na kuenzi Quran Tukufu inayoendelea nchini Tanzania, chini ya Uongozi bora wa Hojjat Al-Islam Dr. Ali Taqavi (Mwenyezi Mungu amuhifadhi) kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya katika uwanja Tablighi, kwa hakika anajituma na kuhakikisha kuwa nuru ya elimu na maarifa ya Quran na ahlulbayt (as) vinazidi kuwaangazia watu wa jamii mbalimbali nchini Tanzania.
-
Tamasha la 30 la Kimataifa la Al-Mustafa la Qur'an na Hadithi - Zanzibar, Tanzania limefanyika kwa mafanikio makubwa
Tamasha hili la Mashindano ya Qur'an Tukufu, ni katika kuhuisha utajo wa Quran Tukufu, na hii ni harakati muhimu ya kuthamini na kuenzi Qur'an Tukufu inayoendelea nchini Tanzania, chini ya Usimamizi na Uongozi bora wa Hojjat Al-Islam Dr. Ali Taqavi (Mwenyezi Mungu Amuhifadhi) kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya katika uwanja Tablighi na khidma kwa Qur'an Tukufu, kwa hakika anajituma na kuhakikisha kuwa nuru ya elimu na maarifa ya Quran na ahlulbayt (as) vinazidi kuwaangazia watu wa jamii mbalimbali nchini Tanzania.
-
Habari Pichani | Mashindano ya Hifdhi ya Qur'an Katika Hawzat ya Mabanati ya Jamiatul - Mustafa (s) - Dar-es-salaam - Tanzania
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Hawzat Zainab (sa) ambayo ni Hawzat ya Mabanati ya Jamiatul - Mustafa (s) - Dar-es-salaam - Tanzania chini ya Uongozi na Usimamizi wa Hojjat al-Islam wal Muslimin, Dr. Ali Taqavi, iliyopo katika maeneo ya Kigamboni - Dar-es-salaam - Tanzania, wakiwa katika Mashindano ya Hifdhi ya Qur'an Tukufu. Hivi sasa mashindano yamefikia katika hatua ya kumpata au kuwapata washindi walio Hifadhi Juzuu 3, Juzuu 7, na Juzuu 30 kabla ya kikao rasmi cha mwisho cha kufanya majumuishi ya Mashindano haya ya Hifdhi ya Qur'an Tukufu na hatimaye kutangaza washindi.
-
Dk. Maarefi akutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Jaft Njawale, Rais wa Umoja wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Augustino Tanzania (SAUTI)
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Mkutano na Rais wa Umoja wa Wanafunzi Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Mwanza. Katika safari yake ya Mwanza, Dk. Maarefi alikutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Jaft Njawale, Rais wa Umoja wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania (SAUT). Mada kuu zilizojadiliwa ni pamoja na kuweka msingi wa programu za pamoja za kitamaduni na kielimu, pamoja na kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano.
-
Mubahatha [Kudurusu kwa Pamoja] - Kwa wanafunzi na watafutaji elimu wote!
Ufahamu huwa na viwango tofauti tofauti, kwa malezi au asili. Wewe ambae ni Mwanafunzi katu usipuuze hichi kipengele cha majadiliano ya kielimu baada ya kupokea maarifa ya mada fulani kutoka kwa Mwalimu.
-
Imam Khamenei afanya ziara muhimu ya kuonesha mafanikio ya sekta binafsi mjini Tehran
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei siku ya Jumanne amefanya ziara katika hafla iliyofanyika ili kuonesha mafanikio ya sekta binafsi.
-
Adui amechanganyikiwa na ana hofu kuhusu maendeleo ya Jamhuri ya Kiislamu / Kudumisha utayari wa hali ya juu na uboreshaji wa maunzi na programu
Ayatullah Khamenei amehusisha hasira za watu wasio na mapenzi mema (wenye nia mbaya) na mabishano yao kwenye vyombo vyao vya habari kuwa ni kuzidisha maendeleo ya Iran na kusema: "Wanabainisha mambo (matakwa) ambayo ni sehemu ya matamanio yao kwa anuani kuwa ni habari na uhakika, na ni lazima kubuni njia za kukabiliana na dhana na propaganda hizi."
-
Habari Pichani | Somo la Fiqh kwa Vitendo
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Katika picha ni Wanafunzi wa Hawzatul-Qaim (a.t.f.s) wakiwa na Mwalimu wao 'Dr.Walid Alisuwailam', akiwa amewawekea Daura muhimu yenye lengo la kuwafundisha namna sahihi ya kuchinja. Daura hii ya Kiilmu itakuwa inaendelea kila siku ya Alhamisi kama Somo la Fiqh kwa Vitendo.
-
"Tumbo ndio Makao Makuu ya Magonjwa Mengi ya Binadamu"
Mtume (saww) ametuambia kuwa "fungeni mpate afya". Na Madaktari wana kitengo maalum cha matibabu kwa kutumia funga, yaani kuna maradhi maalum katika magonjwa ambayo Binadamu tunaugua tiba yake ni kufunga.